loader
Dstv Habarileo  Mobile
Waandishi watakiwa kuepuka habari zinazochochea migogoro

Waandishi watakiwa kuepuka habari zinazochochea migogoro

WAANDISHI wa habari wametakiwa kutumia kalamu zao kuisaidia nchi kupiga hatua za maendeleo na kujiepusha kuandika habari zinazochochea migogoro na kuvuruga amani ya nchi.

Rai hiyo ilitolewa na 

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano mkoani Dodoma, Mchungaji Dk Evance Chande wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.

 Alisema Watanzania wanataka kusikia habari zinazochochea  maendeleo yao na ya nchi badala ya zisizo na tija kwa jamii zinazoashiria uchochezi na uvunjifu wa amani.

 “Taaluma ya uandishi wa habari inathaminiwa na kuaminiwa na Watanzania, kupitia habari zenu kama vile za maendeleo na zinazowagusa watu wote bila kujali itikadi yoyote.” 

"Mategemeo ya wananchi ni kuona waandishi wa habari wanaandika habari zilizo sahihi na sio za kuhamasisha na kuleta migogoro na uvunjifu wa amani nchini," alisema.

Mchungaji Dk Chande alisema Watanzania wanategemea kusikia na kuona habari zinazoandikwa zinasaidia serikali na jamii kuleta maendeleo na kuboresha maisha ya watu badala ya kuyavuruga.

Aidha, aliwataka waandishi wa habari kutumia taaluma yao kufichua maovu kwa lengo la kuisaidia serikali na jamii ambayo mara nyingi yamekuwa yakirudisha nyuma maendeleo ya Watanzania. 

"Bado kuna changamoto kwani baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vinaficha taarifa zinazodumaza maendeleo kutokana na rushwa na kuwafanya hata baadhi ya waandishi kujikuta wakishindwa kuandika ukweli baada ya kupatiwa rushwa," alisema.

 Alisema utoaji wa taarifa za upotoshaji unaofanywa na  baadhi ya waandishi wa habari unasababisha wananchi kukosa matumaini juu ya nchi yao.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/9424b90a1a4033e961003fcb3d6f527c.jpeg

CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali za ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi