loader
Dstv Habarileo  Mobile
Maagizo ya Makamu wa Rais kwa Waziri Makamba

Maagizo ya Makamu wa Rais kwa Waziri Makamba

MAKAMU wa Rais Dk. Philip Mpango ameitaka Wizara ya Nishati kuchukua hatua za haraka kuhakikisha mradi wa kufua umeme katika Bwawa la Julius Nyerere unakamilika kwa wakati.

Akizungumza katika majumuisho ya ziara yake ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa kufua umeme katika Bwawa la Julius Nyerere, Mpango amesema ni muhimu wizara ya Nishati kupitia shirika la umeme nchini (Tanesco) kuimarisha usimamizi, kuongeza wataalam sehemu zenye upungufu pamoja na kuongeza umeme utakaoendesha vyema mitambo ya mkandarasi wakati huu wa ujenzi wa mradi
 

Aidha Makamu wa Rais ameagiza Wizara ya Nishati, Tanesco pamoja na Mkandarasi kupitia upya mpango kazi wa ujenzi wa mradi huo pamoja na kuongeza vitendea kazi na muda wa kufanya kazi ili kuepusha kucheleweshwa kwa mradi.
 

Amesisitiza Serikali inaendelea kutoa fedha kwa wakati ambapo mpaka sasa jumla ya Sh trilioni 2.8 zimelipwa kulingana na mkataba.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/03f30367da9edf9c095154567eb0e31e.jpg

CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali za ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi