loader
Lwandamina: Jeshi lipo tayari, Dube kuikosa Pyramids,

Lwandamina: Jeshi lipo tayari, Dube kuikosa Pyramids,

Kocha Mkuu wa Azam FC, George Lwandamina amesema jeshi lake lipo tayari kwa ajili ya kupambana na Pyramids FC katika mechi ya raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Akizungumza na mtandao huu Lwandamina amesema wanataka kushinda mchezo huo ili kujirahisishia kazi kwenye mchezo wa marudiano ambao utapigwa nchini Misri.

"Tutamkosa Prince Dube pekee bado ni mgonjwa na hatujakuwa naye tangu tuanze msimu, lakini wengine wote wapi fiti kwa ajili ya mchezo wetu wa Jumamosi dhidi ya Pyramids," amesema Lwandamina.

Kocha huyo amesema anatambua ubora waliokuwa nao wapinzani wao na rekodi yao kwenye mashindano hayo  hivyo hilo haliwatishi kwani hata wao ni moja ya timu bora na imepata maandalizi mazuri kuelekea kwenye mashindano hayo.

Azam Fc imefika hatua hiyo baada ya kuiondosha mashindanoni timu ya Hurseed FC ya Somalia kwa jumla ya mabao 4-1 huku mechi zote zikipigwa Tanzania kwenye dimba la Azam Complex  Chamazi Dar es Salaam.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/3e3ed8af12e61b2826398855f8759a27.jpg

ZAIDI ya Vijana 25,000 kutoka ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi