loader
Dstv Habarileo  Mobile
Simbachawene ataka polisi wajizatiti kukabili ugaidi, ukatili kijinsia

Simbachawene ataka polisi wajizatiti kukabili ugaidi, ukatili kijinsia

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amelitaka Jeshi la Polisi liongeze kasi ya mapambano na kujielekeza katika matukio ya ugaidi na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia.

Simbachawene alisema hayo wakati akifunga mafunzo ya uongozi wa Jeshi la Polisi ngazi za Sajenti katika viwanja vya Jeshi la Polisi Ziwani Unguja. Alisema matukio ya ugaidi bado ni tishio hivyo Jeshi la Polisi linawajibika kuchukua aina zote za tahadhari ili nchi iwe salama na matukio hayo ambayo yanaweza kuathiri sekta mbalimbali ikiwemo uchumi na utalii.

Pia alisema kumejitokeza matukio mengi ya vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia katika jamii ikiwemo ubakaji ambavyo vimekuwa vikilalamikiwa na wananchi na Jeshi la Polisi ni sehemu ya majukumu yake kukabiliana kikamilifu.

"Matukio haya ni tishio kwa mustakabali wa maisha yetu na taifa kwa ujumla kwa hiyo Jeshi la Polisi linawajibika kuyafanyia kazi kikamilifu kwa kuongeza ushirikiano na jamii kwa ujumla,’’ alisema.

Alisema mafanikio ya kupambana na matukio hayo na nchi kuwa salama ni pamoja na Jeshi la Polisi kufanya kazi karibu na wananchi kwa kuongeza mashirikiano ya pamoja. Alisema siri kubwa ya Jeshi la Polisi kufanikiwa kupambana na matukio mengi ya uhalifu ni kujenga ushirikiano na wananchi katika kupata taarifa mbalimbali zitakazosaidia katika upelelezi.

"Jeshi la Polisi nendeni mkaimarishe uhusiano mzuri na jamii kwa ujumla ili muweze kupata taarifa mbalimbali zinazohusiana na matukio ya uhalifu,’’ alisema. Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Mohd Haji Hassan alisema matukio ya dawa za kulevya na udhalilishaji wa kijinsia ni makosa ya jinai ambayo wamekuwa wakipambana nayo kila siku ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kazi.

‘’Tumejipanga kupambana na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia ikiwemo ubakaji ambapo dhamana kwa watuhumiwa wa makosa hayo zimefutwa kwa sasa,’’ alisema. Mkuu wa Chuo cha Jeshi la Polisi na uongozi kilichopo Ziwani Unguja, Kamishna Msaidizi Augostino Senga alisema mafunzo waliyoyapata askari polisi yatawawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi na uadilifu wa hali ya juu. Jumla ya askari polisi 1,287 walihudhuria mafunzo hayo kutoka Unguja, Pemba na mikoa mingine ya Tanzania Bara.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/6c20ef014c91de2fd17e298ad49cdc0e.jpeg

CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali za ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi