loader
Dstv Habarileo  Mobile
Mawaziri kujadili umuhimu wa lishe kwa ustawi wa watoto barani Afrika

Mawaziri kujadili umuhimu wa lishe kwa ustawi wa watoto barani Afrika

Mkutano wa 39 wa kawaida wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Umoja wa Afrika umefunguliwa leo Addis Ababa, Ethiopia ambapo pamoja na mambo mengine, Mawaziri watapitia andiko na mikakati ya utekelezaji wa kaulimbiu ya Mwaka 2022 ya“Lishe na Usalama wa Chakula barani Afrika”.

Kaulimbiu hiyo inalenga kusisitiza umuhimu wa lishe bora kwa ajili ya ukuaji na ustawi wa watoto barani Afrika, bara ambalo kwa miaka mingi limekuwa linakabiliwa na uzalishaji mdogo wa chakula.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula anaongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi