loader
Dstv Habarileo  Mobile
Mavunde: Duwasa hamisheni bomba la maji haraka

Mavunde: Duwasa hamisheni bomba la maji haraka

MBUNGE  wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde  ameitaka Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma(DUWASA) kuharakisha zoezi la kuhamisha bomba la maji katika eneo la Kikuyu Kaskazini ili kumruhusu Mkandarasi kuendelea na kazi ya ujenzi wa mitaro na kumaliza kwa wakati.

Mavunde ameyasema hayo leo Oktoba 14,2021 alipotembelea kata ya Kikuyu Kaskazini kukagua ujenzi wa mtaro  wa Kilomita 2.9  wa barabara ya Kinyambwa-Usalama-Michese

Alisema kukamilika kwa mtaro huo kutasaidia kutiririsha maji katika mkondo wake wa asili na kuepusha kutuwama kwa maji ambayo huharibu barabara na kusababisha hadha kubwa kwa wananchi kipindi cha mvua.

Katika ziara hiyo, Mavunde,  ameipongeza serikali chini ya Rais Samia Suluhu kwa kutenga fedha za kuboresha miundombinu ya barabara na madaraja kupitia TARURA ambapo sasa hivi matunda yake yameanza kuonekana.

Alisema wameiombea fedha barabara hiyo kupitia mradi wa TACTIC ili ijengwe kwa kiwango cha Lami.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi