loader
Bilioni 6 kukarabati Mawenzi, kuwa na hadhi kamili ya rufaa

Bilioni 6 kukarabati Mawenzi, kuwa na hadhi kamili ya rufaa

SERIKALI imetenga Sh. bilioni 6,  kwa ajili ya kuboresha Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mawenzi, mkoani Kilimanjaro.

Hayo yamesemwa leo na Rais Samia Suluhu, wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa wodi ya mama na mtoto katika hospitali hiyo.

Rais Samia,  pia ameahidi kuifanya Hospitali hiyo  Mawenzi kuwa na hadhi kamili ya hospitali ya rufaa.

Aidha, Rais Samia amesema tayari Serikali imetoa Sh bilioni tatu ili kuendeleza ujenzi wa wodi hiyo.

Amesema fedha hizo zimetengwa katika Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi na mapambano ya Covid -19 ambao umetokana na mkopo nafuu wa Sh trilioni 1.3 uliotolewa na Shirika la Fedha Duniani (IMF).

“Juzi tulizindua mpango wa matengenezo ya hospitali za rufaa Tanzania nzima, pamoja na vituo vya afya. Hivyo Mawenzi imebahatika na kutengewa Sh bilioni sita na nimeoneshwa Mawenzi inavyotakiwa kuwa,” amesema Rais Samia.

 “Najua kulikuwa na mkwamo kidogo ambao tumeanza kuukwamua na tayari tumeshaingiza sh bilioi 3 nadhani ujenzi utaendelea na zilizobaki tutazimalizia ili jengo likamilike,” amesema Rais Samia, baada ya kuweka jiwe hilo la msingi.

 “Lakini taarifa nyingine nzuri ni kwamba tunajua hospitali yetu ya Mawenzi ni ya siku nyingi na kweli haina hadhi ya kuwa hospitali ya rufaa.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/9134b22993bd8512acd32caee6b581f4.jpg

JESHI la Polisi Mkoa wa Mara linamshikilia Michael ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi