loader
Dstv Habarileo  Mobile
Sabaya na wenzake wahukumiwa  miaka 30 jela

Sabaya na wenzake wahukumiwa miaka 30 jela

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili.

Hukumu hiyo imetolewa baada ya mahakama hiyo, kumkuta na hatia katika kesi iliyokuwa ikimkabili ya unyang’anyi wa kutumia silaha yeye pamoja na wenzake, Sylvester Nyegu na Daniel Mbura

Hukumu hiyo imetolewa leo Ijumaa, 15 Oktoba15,  2021 na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Odira Amworo.

Hakimu Mwandamizi Amworo amesema, mahakama imethibitisha pasi na shaka Sabaya alitenda makosa hayo.

Kabla ya kutoa adhabu, Hakimu Odira alimpa fursa Sabaya ya kusema chochote ambapo aliiomba mahakama imuonee huruma kwani siyo yeye bali alikuwa anatekeleza maagizo ya mamlaka yake ya uteuzi na ana mchumba ambaye walikuwa wafunge ndoa kwani mahari amekwisha lipa.

Sabaya na wenzake walikuwa wanatuhumiwa kuvamia na kufanya unyang’anyi wa kutumia silaha wa zaidi ya Sh. 2.7 milioni, katika duka la Mohamed Saad, Februari 9, 2021.

Kesi hiyo, ilisikilizwa mfululizo kuanzia Julai 19,hadi 24 Agosti 2021 baada ya Sabaya na wenzake, kusomewa maelezo ya awali ya kesi hiyo mhakamani hapo, Julai 16, 2021.

Sabaya na wenzake alifikishwa mahakamani baada ya Rais Samia Suluhu, kutangaza kumsimamisha kazi Mei 13, 2021 ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zilizokuwa zinamkabili.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/2261589afa3ac31938087c10ad9a5d8c.png

SERIKALI imepanga kujenga ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi