loader
Dstv Habarileo  Mobile
Chakula bwerere nchini, utapiamlo tishio

Chakula bwerere nchini, utapiamlo tishio

WAKATI dunia inaadhimisha Siku ya Chakula Duniani leo, Tanzania imejitosheleza kwa chakula kwa asilimia 100 na kuwa na ziada ya tani takribani milioni nne.

Hayo yalibainishwa na Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, alipozungumza na HabariLeo jana.

Bashe alisema kwa muda mrefu sasa Tanzania imejitosheleza kwa chakula kwa asilimia 100 na hakuna upungufu wa chakula hapa nchini.

“Mahitaji yetu ya chakula kwa mwaka ni tani milioni 13. Kama nchi tumejitosheleza kwa chakula kwa asilimia 100 na tuna ziada ya tani karibu milioni nne. Changamoto kwenye chakula ni suala la lishe, mikoa inayoongoza kwa utapiamlo ni mikoa inayozalisha chakula kwa wingi,” alisema Bashe.

Alisema moja ya mipango ya serikali ni kuwekeza zaidi kwenye miundombinu ya umwagiliaji, maghala, upatikanaji wa mitaji kwa urahisi kwenye sekta ya kilimo kwa kuwa chakula pia ni biashara.

“Kwetu chakula ni biashara pia, kwa hiyo tunazalisha kwa ajili ya mahitaji yetu ya ndani na pia tunazalisha kwa ajili ya kuuza. Tumekuwa tukiuza mazao mbalimbali ya chakula ndani na nje ya Afrika Mashariki. Moja ya biashara kubwa duniani katika miaka mitatu ijayo itakuwa biashara ya chakula,” alisema Bashe.

Alisema jambo jingine ambalo serikali inapambana nalo ni kuwekeza kwenye suala la hifadhi ya chakula cha dharura.

Kwa mujibu wa Bashe, serikali imeongeza uhifadhi wa chakula cha dharura kutoka tani 200,000 hadi tani 520,000.

Alisema serikali inafanya jitihada ya kupunguza gharama za pembejeo, viuatilifu, dawa na mbolea, hivyo wakulima wanapaswa kuzalisha siyo tu kwa ajili ya chakula bali kwa biashara pia.

Katika taarifa yake ya kila wiki hivi karibuni, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, alisema kilimo kinachangia asilimia 25 kwenye Pato la Taifa na kinaliingizia taifa fedha za kigeni Dola za Marekani bilioni moja, sawa na Sh

trilioni 2.2.

FAO Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) limesema katika mtandao wake kuwa watu zaidi ya bilioni tatu sawa na takribani asilimia 40 ya watu ulimwenguni hawamudu lishe bora.

Pia lilisema watu takribani bilioni mbili duniani wana uzito uliozidi au wanene kupita kiasi kutokana na lishe isiyo na mpangilio au maisha ya kukaa tu.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/dd6e77a01b088fc170f5d009cb232512.jpg

SERIKALI imepanga kujenga ...

foto
Mwandishi: Matern Kayera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi