loader
Abambwa akitengeneza, kuuza vitambulisho feki vya NIDA

Abambwa akitengeneza, kuuza vitambulisho feki vya NIDA

JESHI la Polisi mkoani Pwani linawashikilia watu wawili kwa tuhuma mbalimbali mmoja akidaiwa kutengeneza vitambulisho vya taifa vya NIDA na kuviuza Sh 10,000 kila kimoja.

 

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Wankyo Nyigesa alisema kwenye tukio la kwanza lililojiri Oktoba 12, mwaka huu, Abdul Seleman (27) mfanyabiashara wa stationery na mkazi wa Visiga kwa Kipofu wilayani Kibaha alikamatwa kwa tuhuma za kutengeneza nyara za serikali.

Alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa kwa ushirikiano wa polisi na vyombo vingine vya dola ambapo alikuwa akiuza vuitambulisho feki vya Nida kwa Sh 10,000. Vitambulisho hivyo kwa kawaida hutolewa bure na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Aidha alise- ma mtuhumiwa huyo alikutwa na vitambulisho viwili ambavyo tayari alikuwa amevitengeneza.

Alisema Abdul atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

Katika tukio la pili, mkazi mmoja wa Kwa Mfipa wilayani Kibaha, Peter Baziro anayetambulika pia kama Pius Nducha anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuwatapeli watu kuwa anauza viwanja.

Alisema kuwa mtuhumiwa alikamatwa baada ya kumtapeli Jenifa Asa kiasi cha Sh milioni 1.4 akidai angemuuzia kiwanja chenye ukubwa wa 20 kwa 20.

“Mtuhumiwa mbali ya kutapeli viwanja amekutwa akidai anauza magari huku akiwa na hati za kughushi zikiwemo za mauziano na za viwanja. Mpaka tunamkamata tayari alikuwa amewatapeli watu mbalimbali,” alisema Nyigesa.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/69ad1febe245c4c9f504c919f6da3ffa.jpeg

JESHI la Polisi Mkoa wa Mara linamshikilia Michael ...

foto
Mwandishi: John Gagarini, Kibaha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi