loader
Ruvuma kuzalisha tani 25,000 za korosho

Ruvuma kuzalisha tani 25,000 za korosho

MKOA wa Ruvuma kupitia Chama Kikuu cha Ushirika Wilaya ya Tunduru (Tamcu Ltd), katika msimu wa 2021/2022 unatarajia kuzalisha na kuuza tani 25,000 za korosho.

Meneja wa Bodi ya Korosho Wilaya ya Tunduru, Shauri Mokiwa alisema uzalishaji huo wa takribani kilogramu milioni 25, ni ongezeko la asilimia 38 ikilinganishwa na uzalishaji wa msimu uliopita.

Msimu wa 2020/2021 walizalisha kilogramu 15,410,551 zilizokusanywa na kuuzwa kupitia stakabadhi ghalani.

Alisema katika msimu huo wa 2020/2021, uzalishaji ulishuka ikilinganishwa na 2019/2020 ambao jumla ya kilogramu 24,624,284 zilikusanywa na kuuzwa.

Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Julius Mtatiro aliwataka wanunuzi kujiepusha kununua korosho kwa njia zisizo halali maarufu kama kangomba.

Mtatiro alisema serikali itahakikisha korosho zote zilizozalishwa katika msimu wa kilimo 2021 zinauzwa kwa mfumo wa stakabadhi ghalani na si vinginevyo.

Mtatiro ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya, alionya watumishi na wafanyabiashara dhidi ya kununua korosho kinyume na mfumo wa stakabadhi ghalani.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/b8d48d87cb74c743aa7b6384c0d81bed.jpeg

JESHI la Polisi Mkoa wa Mara linamshikilia Michael ...

foto
Mwandishi: Muhidin Amri, Tunduru

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi