loader
Kagera Sugar yasaka rekodi nyumbani

Kagera Sugar yasaka rekodi nyumbani

KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Francis Baraza amesema wanataka kuanza kuweka rekodi ya matokeo mazuri kuanzia mchezo wa leo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

Akizungumzia mchezo huo jana, Baraza alisema wameanza vibaya ligi kutokana na ushindani lakini wamejipanga wakitaka matokeo mazuri kwenye uwanja wa nyumbani.

Alisema wanachukulia kila mchezo kama fainali kwao ili kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.

“Vijana wameonesha morali kwenye mazoezi, tunajua tulifanya makosa michezo iliyopita hatukufanya vizuri, tumerekebisha na lengo ni kuanza kushinda michezo yetu yote ijayo,” alisema.

Baraza alisema wanajua Mbeya City ni timu nzuri na ina kocha mzuri pia, wameanza ligi wakiwa bora ila na wao wanataka washinde mchezo huo ili kujiwekanafasi nzuri.

Kagera Sugar imecheza michezo miwili na kati ya hiyo imepoteza mmoja dhidi ya Yanga bao 1-0 na kupata sare dhidi ya Namungo ya bao 1- 1. Inashika nafasi ya 11.

Kwa upande wa Mbeya City, inashika nafasi ya nne baada ya kushinda mchezo mmoja dhidi ya Tanzania Prisons bao 1-0 na kutoka sare mchezo uliopita dhidi ya Mbeya Kwanza mabao 2-2.

Mchezo mwingine utakaochezwa leo mbali na huo ni Geita Gold FC dhidi ya Mtibwa Sugar.

Geita baada ya kupoteza michezo miwili ya ugenini dhidi ya Yanga bao 1-0 na Namungo mabao 2-0 inarejea nyumbani kwenye uwanja wake wa Nyankumbu na wamedhamiria kuutumia kupata matokeo mazuri.

Inakutana na Mtibwa Sugar ambao pia hawajaanza ligi vizuri baada ya kupoteza mchezo mmoja dhidi ya Mbeya Kwanza bao 1-0 na kupata suluhu dhidi ya Tanzania Prisons.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/f4086e60953631c65a675afc60aa9d3f.jpeg

MAKOCHA wa Simba Pablo Franco na wa Yanga, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi