loader
Mayele: Ligi ya Bara ngumu

Mayele: Ligi ya Bara ngumu

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Fiston Mayele ameimwagia sifa Ligi Kuu ya Tanzania Bara akisema ni ngumu na ina ushindani mkubwa zaidi ya ligi ya kwao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

Mayele ambaye ndio mshambuliaji tegemezi kwenye kikosi cha Yanga, mpaka sasa hajaifungia timu yake bao katika mechi mbili alizocheza.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mayele alisema sababu ya kutofunga mpaka sasa ni ushindani mkali aliokutana nao kutoka kwa mabeki wa timu alizokutana nazo, ambao ulimnyima nafasi ya kufanya kile alichokuwa anakifanya akiwa timu yake ya zamani ya AS Vita.

“Nikweli ligi ya Tanzania ni ngumu zaidi ya hata Congo, nimeona katika mechi mbili nilizocheza mabeki wamekuwa wakinikaba hawanipi hata nafasi, lakini kitu kingine nilichokiona ni waamuzi kutokuwa makini sana,” alisema Mayele.

Mshambuliaji huyo alisema pamoja na ushindani huo, lakini anaamini yeye ni bora na atalidhihirisha hilo siku zijazo sababu ligi bado inaendelea na taratibu ameanza kuzoea mazingira ya ushindani kutoka kwa mabeki wa timu zinazoshiriki Ligi Kuu.

Alisema kushindwa kufunga bao kwenye mechi mbili za ligi kumemuumiza sababu 

alipata nafasi kadhaa lakini uharaka wa kutaka kufunga ndio ulichangia ashindwe kuzitumia nafasi hizo na kusababisha timu yake kupata ushindi mdogo ambao alisema siyo mbaya sababu wamepata pointi

tatu muhimu.

Mayele ni miongoni mwa wachezaji watano raia wa Congo waliosajiliwa na Yanga msimu huu wengine ni Jesus Moloko, Djuma Shaban, Yannick Bangala na Heritier Makambo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/e33a02d4ab8b4aa563897e5bbb72a2d1.jpeg

MAKOCHA wa Simba Pablo Franco na wa Yanga, ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi