loader
Maabara kubwa kujengwa KCMC

Maabara kubwa kujengwa KCMC

HOSPITALI ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini KCMC  ipo kwenye ujenzi wa Maabara ya kisasa, ambayo itakuwa na uwezo wa kuchakata sampuli mbalimbali na kutoa majibu haraka.

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini Dk Fredrick Shoo, amesema mbali na maabara hiyo pia kutakuwa na vyumba nane vya upasuaji wa uti wa mgongo, ubongo na mishipa ya fahamu.

“Tunamshukuru Balozi wa Ujerumani, Abdallah  Posi amekuwa kiungo muhimu kwa kuwaunganisha na wafadhili kwa ajili ya kupata msaada wa kufanikisha ujenzi wa miundo mbinu hii,” alisema Dk Shoo.

Aidha askofu Shoo amesema pia kuna ujenzi wa vyumba nane vya upasuaji ikiwemo vya uti wa mgongo, ubongo na mishipa ya fahamu.

Aidha alitoa ombi kwa Rais Samia Suluhu, kuwapatia watumishi mara miradi hiyo itakapokamilika.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/6fb17c5553e2094d34af4eea443ba254.png

JESHI la Polisi Mkoa wa Mara linamshikilia Michael ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi