loader
|Rais Mwinyi ateua Kaimu Jaji Mahakama Kuu

|Rais Mwinyi ateua Kaimu Jaji Mahakama Kuu

RAIS  wa Zanzibar,  Dk Hussein  Ali Mwinyi,  amefanya uteuzi wa nyadhifa mbalimbali katika Mahakama Kuu, Wizara na Taasisi za Umma.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Zena Said, inasema Rais Mwinyi amemteuwa  Jaji Khamis Ramadhani Abdallah kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu Zanzibar

Pia amemteua Masoud Abdallah Balozi kuwa Katibu wa Rais wa Zanzibar ofisi ya Rais Ikulu.

Aidha amemteua Dk Haji Mwevura Haji kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya ushauri ya Maabara ya Mkemia Mkuu, huku Shaaban Hassan Haji,  akiteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Uendeshaji wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi.

Taarifa hiyo imesema uteuzi huo unaanzia leo Oktoba 20, 2021 ambapo kesho saa tatu Oktoba 21, Rais  Mwinyi atamuapisha Kaimu Jaji Mkuu

Pia atawaapisha Kapteni Khatib Khamis Mwadin, Naibu Mkuu wa Kikosi Maalum cha Kuzuia Magenzo (KMKM) aliyeteuliwa Oktoba 8, 2021 na Suleiman Abdulla Salim, Katibu Tume ya Utangazaji ambae aliteuliwa Septemba 2021

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/78c614f947cbcf05b1624355c558657c.jpg

JESHI la Polisi Mkoa wa Mara linamshikilia Michael ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi