loader
Mpango akaribisha  wawekezaji wa Ufaransa

Mpango akaribisha wawekezaji wa Ufaransa

MAKAMU wa Rais, Dk Philip Mpango amekaribisha wawekezaji kutoka Ufaransa kwa kuwaeleza kuwa Tanzania ni salama kuwekeza, ina rasilimali na fursa nyingi.

Dk Mpango alisema serikali imeendelea kukabili changamoto za kiuchumi zilizosababishwa na janga la ugonjwa wa Covid-19 na kwa sasa inatoa chanjo ili kuwalinda wananchi.

Alisema hayo Ikulu Dar es Salaam alipokutana na kuzungumza na Waziri Biashara za Kimataifa na Uwekezaji wa Ufaransa, Franck Riester.

Dk Mpango alisema Ufaransa imekua miongoni mwa wadau wakubwa wa uwekezaji na maendeleo kwenye sekta mbalimbali nchini Tanzania.

Alitaja miongoni mwa sekta hizo kuwa ni miundombinu, elimu na maji. Aliwakaribisha wawekezaji kutoka nchini huo waje kuwekeza kwenye sekta ya afya hasa ujenzi wa viwanda vya dawa, sekta ya utalii na nishati.

Mazungumzo ya viongozi hao yalihudhuriwa wakiwemo mawaziri kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Srikali ya Mapinduzi Zanzibar na Balozi wa Ufaransa nchini, Nabil Hajlaouvi.

Riester aliwasilisha salamu na mwaliko wa Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Alisema Ufaransa inatambua jitihada za Serikali ya Tanzania kuboresha mazingira ya biashara na kuleta usawa wa kijinsia.

Alisema Ufaransa imedhamiria kuongeza ushirikiano na Tanzania kwa manufaa ya nchi hizo na alitoa mfano wa kuanzishwa kwa usafiri wa ndege wa moja kwa moja kutoka jijini Paris hadi Zanzibar.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/0c15c976b58d8d2caf779bc7355506a2.jpg

JESHI la Polisi Mkoa wa Mara linamshikilia Michael ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi