loader
Jengeni taifa la kidigitali

Jengeni taifa la kidigitali

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Posta nchini, Macrice Mboda, ameelezea umuhimu wa kujenga taifa la kidijitali ili kukabiliana na changamoto wanazokutana nazo wananchi katika kupata huduma katika taasisi mbalimbali zikiwemo za serikali.

Akizungumza Katika Kongamano la Tehama linalofanyika jijini Arusha, Mboda amesema ili kukabiliana na changamoto hizo shirika la posta liliona umuhimu wa kuanzisha kituo cha huduma kitakachowawezesha wananchi kupata huduma mbalimbali katika kituo kimoja.

Serikali ya Awamu ya sita imeamua kuanzisha mradi huo ambao unatarajiwa kuenea nchi nzima unajulikana kama  HUDUMA PAMOJA ambapo kwa mwaka huu umeanza kuhudumia wananchi katika mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma.

“Kumekuwa na mzunguko mkubwa wa kupata huduma ikiwemo vitambulisho vya taifa, paspoti au leseni za biashara ambapo mwananchi anatakiwa kwenda katika kila idara husika ambazo ziko mahali tofauti ikiwemo kufanya malipo ya huduma hizo na hivyo kusababisha misongamano na usumbufu usio na lazima” alisema Mbado

Katika mradi huo kutakuwa na huduma mbalimbali ambazo ni pamoja ile ambayo mwananchi ataweza kujihudumia mwenyewe kupitia simu yake au kifaa chochote cha mawasiliano ya kielektroniki ijulikanayo kama huduma portal.

Huduma nyingine muhimu inajulikana kama Huduma Pay, ambapo mwananchi anaweza kufanya malipo ya huduma mbalimbali za serikali katika kituo kimoja na hivyo kuokoa muda wa kufanya shughuli nyingine za maendeleo.

Akizungumzia mradi wa huduma hizo, Mkurugenzi huyo wa Shirika la Posta amesema serikali imechagua shirika hilo kutekeleza mradi huo kutokana na ukweli kuwa shirika la posta ndio taasisi iliyo karibu na wananchi kuliko nyingine.

Aidha Mboda aliitaja sababu nyingine kuwa ni muunganiko wa mtandao wa mashirika ya posta duniani ambapo Tanzania ni mjumbe wa Umoja wa Posta duniani (CPU), na hivyo kuwa rahisi mwananchi kupata huduma kutoka nchi zilizo kwenye mtandao huo zikiwemo China, Japan, Misri, Tunisia na Afrika Kusini.

Pia nchi za Kenya, Botswana, Dubai, Marekani, Canada na nyingine ambazo umoja huo unahamasisha nchi wanachama kutoa huduma kwa wananchi wake kupitia mtandao mpana wa posta duniani.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/e0dd62d082b295ba86591d8a4fb40452.jpg

JESHI la Polisi Mkoa wa Mara linamshikilia Michael ...

foto
Mwandishi: Adam Lutta, Arusha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi