loader
Mfumuko wa bei kupanda asilimia 4 Uingereza

Mfumuko wa bei kupanda asilimia 4 Uingereza

Mfumuko wa bei wa bidhaa nchini Uingereza unatarajiwa kupanda kutoka asilimia 3.1 msimu huu wa baridi hadi asilimia 4 kufikia Septemba 2022, kwa mujibu wa Waziri wa Fedha, Rishi Sunaki.

Akizungumza bungeni wakati wa uwasilishaji wa bajeti ya mwaka 2021, Waziri wa Fedha, Richi Sunak amesema mfumuko wa bei ulikuwa asilimia 3.1 mwezi Septemba na kuna uwezekano wa kupanda zaidi.

“Itakuwa ni kutowajibika kwa mtu yeyote kujifanya kuwa tunaweza kutatua hili mara moja"amesema Sunak na kuongeza kuwa “Serikali itachukua hatua pale itakapoweza.”

Akitoa taarifa yake ya bajeti, Sunak ametoa taarifa njema za ukuaji wa uchumi na kuwaambia wabunge kuwa Ofisi ya Uwajibikaji wa Bajeti (OBR) inaamini kuwa upungufu mdogo wa kiuchumi ulitokana na janga la corona.

Kwa sababu hiyo, utabiri wa hivi wa ukuaji wa OBR unatarajia uchumi sasa kukua kwa kasi zaidi, kwa asilimia 6 mwaka 2022 - na kisha kwa kiwango cha asilimia 2.1, asilimia 1.3 na asilimia 1.6 katika miaka inayofuata.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/0860c2577b3f91f10906be9bdf79185a.jpg

UGANDA imekubali kuongeza maradufu idadi ya ...

foto
Mwandishi: WESTMINISTER, Uingereza

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi