loader
Waziri Mkuu Uingereza akubali kuvaa tena barako

Waziri Mkuu Uingereza akubali kuvaa tena barako

KWA zaidi ya mwezi mmoja sasa, Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson amekuwa akikataa kuvaa barakoa, hatimaye leo Boris ameingia bungeni kusikiliza Bunge la Bajeti akiwa amevaa barakoa.

Boris amelazimika kuvaa barakoa kutokana na sheria mpya zilizowekwa kwa wafanyakazi wa bunge jana Jumanne kabla ya hotuba ya bajeti, zikiwahitaji kuvaa barakoa, ingawa haiwaamuru wabunge kufanya hivyo.

Idadi ya wabunge na viongozi wengine waliova barakoa ilikuwa kubwa zaidi kuliko ilivyokuwa katika wiki za hivi karibuni.

Licha ya wingi wa wabunge kuvaa barakoa, wasimamizi watatu wa mbele walionekana bila barakoa walipokuwa wameketi wakati kansela, Rishi Sunak, akiwasilisha bajeti.

Viongozi hao ni Katibu Mkuu wa Scotland, Alister Jack, Katibu wa Kazi na Pensheni, Therese Coffey; na kiongozi wa House of Commons, Jacob Rees-Mogg.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/bb757656fafbbb7db2c4565ebc764c6a.jpg

UGANDA imekubali kuongeza maradufu idadi ya ...

foto
Mwandishi: WESTMINISTER, Uingereza

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi