loader
Necta yataja vigezo kupanga kidato cha kwanza

Necta yataja vigezo kupanga kidato cha kwanza

OFISI ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), imetangaza kuwa kuanzia sasa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), ndio litakaohusika na uchaguzi na upangaji wa wanafunzi wa kidato cha kwanza na cha tano.

Awali, jukumu hilo lilikuwa chini ya Ofisi hiyo ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

Kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde, baraza hilo limepewa jukumu la kuratibu na kusimamia uchaguzi wa wanafunzi kujiunga na kidato cha kwanza pamoja na wale wanaojiunga na kidato cha tano.

Dk Msonde alisema jukumu hilo walilokabidhiwa kwa upande wa wanafunzi wa kidato cha kwanza, waliopangiwa kujiunga na kidato hicho, Necta itawapangia katika shule zenye makundi makubwa mawili; shule za bweni na kutwa.

Alisema kwenye shule za bweni ziko pia katika makundi matatu ambayo ni shule za bweni maalumu kama vile Kilakala, Mzumbe, Ilboru, Msalato na nyinginezo, shule za ufundi kama vile Moshi Technical na Iringa, shule za bweni za kitaifa kama vile Kilosa na Korogwe.

Dk Msonde alisema kwa upande wa shule za kutwa, zipo nyingi nchini ambazo wanafunzi wanakwenda shule kutoka nyumbani na kurejea nyumbani na kubainisha kuwa wanafunzi wengi wanaojiunga na kidato cha kwanza watapangiwa shule hizo za kutwa.

Alieleza kuwa ili wanafunzi hao wa kidato cha kwanza na cha tano wapangiwe shule za kujiunga, wanatakiwa watimize vigezo mbalimbali lakini kigezo kikubwa ni ufaulu wa mitihani.

“Kwa hiyo baraza litakuwa na wajibu mkubwa wa kupanga wanafunzi waliofaulu katika ngazi zote za mikoa na halmashauri. Na majina yote ya wanafunzi yatapangwa kuanzia yule aliyefaulu kwa alama za juu mpaka za chini,” alisema mtendaji huyo wa Necta.

Alifafanua kuwa hatua hiyo itasaidia wanafunzi hao kupangwa kwenye shule kulingana na ufaulu wao na kubainisha kuwa wataanza na kundi la wanafunzi wenye ufaulu wa juu na kupelekwa kwenye shule zenye ufaulu wa juu kama vile Kilakala, Mzumbe na Ilboru.

“Baada ya shule hizo kukamilisha kujaza wanafunzi kulingana na ufaulu wao, baraza litapanga ufaulu unaofuata kwenye shule za ufundi, pia watapanga ufaulu unaofuata kwenda kwenye shule za bweni za kawaida na kundi litakalofuata la waliofaulu wote watapangwa kwenye shule za sekondari za kutwa,” alieleza.

Aidha, alisema pia watakuwepo watahiniwa wenye mahitaji maalumu ambao watapangwa kulingana na nafasi zilizopo na shule zinazoweza kuwapokea kutokana na uhitaji wao maalumu.

Dk Msonde alisema kwa mwaka huu, mtihani wa darasa la saba kwa mara ya kwanza wanafunzi walifanya mitihani sita badala ya matano waliyokuwa wakiyafanya miaka iliyotangulia.

“Wakati wakifanya masomo matano katika miaka iliyotangulia ufaulu ulikuwa ni alama 100 kati ya 250 walizotakiwa kuzipata lakini mtihani wa darasa la saba wa mwaka huu 2021 ufaulu sasa utakuwa ni alama 121 hadi alama 300,” alisema Dk Msonde.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/0cffd7198ea66c97f24c8375b08a30ba.jpeg

JESHI la Polisi Mkoa wa Mara linamshikilia Michael ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi