loader
Balozi Uingereza apewa siku 21 kuondoka Sudan

Balozi Uingereza apewa siku 21 kuondoka Sudan

Taifa la Sudan limempa siku 21 Balozi wa Uingereza nchini humo, Giles Lever kuondoka kwa hiara yake katika Mji Mkuu wa Khartoum na kurejea nchini kwake.

Hatua hiyo imekuja baada ya siku kadhaa zilizopita balozi huyo kudai kuwa Uingereza inalaani vikali hatua za Jeshi la Sudan kumuweka kizuizini Waziri Mkuu, Abdalla Hamdok.

Kiongozi mmoja wa jeshi la Sudan Alhamisi iliyopita alitangaza kuwa, Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya nchi hiyo amewafukuza mabalozi wasiopungua sita wakiwemo mabalozi wa nchi hiyo huko Marekani katika Umoja wa Afrika (AU) na nchini Ufaransa kwa hatua yao ya kulaani mapinduzi yaliyofanywa na jeshi la Sudan. 

Shirika la habari la Associated Press limeripoti kuwa wanadiplomasia sita wa Sudan wamefukuzwa katika nafasi zao za ubalozi kwa kosa la kumuunga mkono Waziri Mkuu Abdullah Hamdok aliyeondolewa madarakani katika mapinduzi hayo ya jeshi.
Wananchi wa Sudan wameendelea na maandamano katika miji ya Sudan na miji mingine mbalimbali duniani wakitangaza upinzani wao dhidi ya mapinduzi ya kijeshi nchini humo.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/1f2a2852718621f50d66e04a8f0004ed.jpg

UGANDA imekubali kuongeza maradufu idadi ya ...

foto
Mwandishi: KHARTOUM, Sudan

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi