loader
#COP26 Waziri Mkuu Uingereza atahadharisha matumizi ya magari ya mafuta

#COP26 Waziri Mkuu Uingereza atahadharisha matumizi ya magari ya mafuta

WAZIRI Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema ulimwengu unahitaji kuweka mikakati madhubiti kuondokana na matumizi ya nishati ya mafuta na gesi ikiwa ni pamoja na matumizi ya magari yanayotegemea nishati hiyo kama mkakati wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Akihutubia hafla ya ufunguzi wa mkutano wa 26 wa Umoja wa Mataifa unaohusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP26), Johnson amesema, masaa yanayoyoma na kwamba kila mtu ni lazima afanye zaidi na kutoa ahadi zaidi.

“Ahadi hizo zinahitaji kujumuisha hatua kama vile kuachana na matumizi ya mafuta, kutumia magari ya umeme na kupanda mamilioni kama sio trilioni ya miti kote ulimwenguni,” amesema.

Nakusisitiza, “sote tunahitaji kutafakari jinsi tutakavyoweza kusaidia ulimwengu mzima hasa nchi zinazoendelea kukubari juu ya mpango huu,” amesema.

Mkutano huo ulioanza rasmi leo unahudhuriwa na viongozi wakubwa. Rais Samia Suluhu Hassan anashiriki mkutano huo na anatarajiwa kuhutubia hapo kesho, Novemba 2. Viongozi wengine walioshiriki nipamoja na Rais wa Marekani Joe Biden. Rais wa Urusi Vladimir Putin hatashiriki mkutano huo.

Akihutubia mkutano huo, Biden ameonya ulimwengu ikiwa utashindwa kuchukua hatua sasa kukabiliana na janga la mabadiliko ya tabianchi akirejea madhira yaliyoletwa na UVIKO-19 ambayo yameweza kuvuka mipaka na kusulubu ulimwengu mzima.

Amesema “ingawa ni janga bado kuna fursa nzuri sio tu kwa marekani bali sisi sote.”

Biden anaamini kuwa fursa ya kujenga ulimwengu wenye usawa na kutumia nishati safi, mambo ambayo yanaweza kutengeneza mamilioni ya ajira zinazolipa vizuri kote ulimwenguni.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/a0a6580ae08b9a1b40f4131e510871d9.jpeg

UGANDA imekubali kuongeza maradufu idadi ya ...

foto
Mwandishi: NA MWANDISHI WETU

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi