loader
#COP26 India kuachana na uzalishaji gesi chafuzi ifikapo 2070

#COP26 India kuachana na uzalishaji gesi chafuzi ifikapo 2070

INDIA imetangaza kuachana na uzalishaji gesi chafu ifikapo 2070 mpango ambao unakidhana na lengo la mkutano wa Umoja wa Mataifa unaohusu mabadiliko ya tabianchi COP26 unaotaka nchi kufikia sifuri ifikapo 2050.

Hii ni mara ya kwanza kwa India kutoa ahadi hiyo. Nchi za Umoja wa Ulaya na Marekani zimepanga kufikia lengo hilo ifikapo 2050.

Akihutubia katika mkutano ulioanza leo Glasgow, Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi amesema ahadi hiyo ni moja ya mikakati inayotekelezwa na nchi yake. Ahadi nyingine ni pamoja na kufikia asilimia 50 ya matumizi ya nishati jadidifu ifikapo 2030 na kupunguza uzalishaji wa kaboni kwa tani bilioni moja.

India ni nchi ya nne kwa uzalishaji wa gesi chafu. Umoja wa Ulaya (EU) unaongoza ukifuatiwa na Marekani na nchi ya tatu ni China. Hata hivyo, Rais Xi Jingping wa China amesema wakati akihutubia kwa njia ya mtandao kuwa nchi yake itafikia lengo hilo mwaka 2060.

Shirika la Utangazaji BBC limenukuu ripoti ya mwaka 2019 ikionyesha kuwa uzalishaji wa kaboni kwa India bado uko chini ukilinganisha na nchi kama marekani kutokana na idadi kubwa ya watu.

BBC imeandika kuwa katika ripoti hiyo, mtu moja kwa India alizalisha tani 1.9 za kaboni ukiringanisha na tani 15.5 kwa marekani ama tani 12.5 kwa Urusi.

Lengo la kufikia sifuri halisi ama kutokuwa na kaboni inamaanisha kutoongeza kiwango cha gesi chafuzi katika angahewa ifikapo 2050.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/377b01eb0558fe47c5b5b18e1376e007.jpeg

UGANDA imekubali kuongeza maradufu idadi ya ...

foto
Mwandishi: NA MWANDISHI WETU

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi