loader
Watu 99 wafariki baada ya lori la mafuta kuanguka

Watu 99 wafariki baada ya lori la mafuta kuanguka

WATU 99 wamepoteza maisha baada ya loli la mafuta kuanguka na kuwaka moto katika Mji Mkuu wa Freentown nchini Sierra Ijumaa.

Naibu Waziri wa Afya nchini Sierra Leon, Amara Jambai aliliambia shirika la habari la Reuters kuwa watu 100 wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali tofauti.

Kwa mujibu wa Meya wa Freetown, Yvonne Aki-Sawyerr waathiriwa wa tukio hilo ni waliokimbilia kuchota mafuta baada ya gari kuanguka. 

Meya huyo amesema kiwango cha uharibifu wa mali katika eneo la tukio hakijajulikana na kuongeza kuwa polisi walikuwa kwenye eneo la tukio kusaidia maafisa wa usimamizi wa maafa.

Aidha, Mkuu wa Shirika la Kitaifa la Kudhibiti Maafa, Brima Sesay amesema majeruhi ni wengi na huenda ikiwa zaidi ya ilivyoripotiwa. "Tuna majeruhi wengi sana, ajali ilukuwa mbaya, mbaya." Amesema Sesay.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/b952394874f3a5d0152e5fc195048147.jpg

RAIS Mstaafu wa Awamu ya ...

foto
Mwandishi: FREETOWN, Sierra Leon

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi