loader
OUT kinara ubora Afrika, cha 13 duniani

OUT kinara ubora Afrika, cha 13 duniani

CHUO Kikuu Huria Tanzania (OUT), kinashika nafasi ya kwanza kwa ubora Barani Afrika kati ya Vyuo Vikuu Huria 16 vilivyopo jambo linaloleta heshima kubwa kwa taifa.

Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Elifas Bisanda amesema hayo alipokuwa akizungumza na HabariLeo kuhusu chuo hicho katika kipindi hiki cha kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania.

Akizungumzia ubora wake kidunia amesema, duniani vyuo vikuu huria vipo 146, OUT kinashika namba 13 hivyo kukifanya kiwe juu kiulimwengu.

“Walichukua vyuo vyote vya Tanzania ambavyo idadi yake vipo karibia 54, sisi OUT ni namba sita kwa ubora. Mimi nahisi kama wanaofanya tathmini wengi wangetuangalia vizuri zaidi huenda tungekuwa namba moja,” amesema.

Amesema sababu mojawapo inayowafanya kuwa chuo bora, ni mifumo yao ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), waliyonayo kwani hakuna mtu mwingine aliyonayo ndio maana mitahani ya chuo hicho haiwezi kuvuja.

“Mwalimu wa somo mwenyewe hajui mtihani wake utakaofanywa na wanafunzi, ndio maana wanafunzi hao sasa hivi wanasoma sana kuliko zamani,” amesema.

Mbali na kuwa bora kitaaluma, katika miaka ya 60 ya uhuru kama chuo wameshiriki kuongeza rasilimali watu kwani mpaka sasa zaidi ya wahitimu 46,000 wamehitimu chuoni hapo tokea chuo hicho kilipoanza miaka 30 iliyopita kwa ngazi ya cheti, diploma na shahada.

“Ukichukua idadi hiyo ni kubwa ukilinganisha tulipotoka kama nchi wakati tulipopata uhuru kwani kipindi hicho kulikuwa na madaktari wenye shahada wachache lakini leo hii wamezalishwa wengi, kwenye taaluma za ualimu, uchumi, sayansi na mazingira na nyinginezo,” amesema.
 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/90fa09277b9b02b8d7fcdc55d9fbc312.png

JESHI la Polisi Mkoa wa Mara linamshikilia Michael ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

1 Comments

  • avatar
    Ngogomela
    11/11/2021

    Positive development

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi