loader
Roma ataka wasanii kuacha amapiano

Roma ataka wasanii kuacha amapiano

RAPA wa Tanzania, Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki’ amewaasa wasanii wenzake kutumia miezi miwili kuimba mara ya mwisho staili ya amapiano.

Kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Twitter, nyota huyo aliyeko Marekani kwa sasa, aliandika ujumbe kuwataka wasanii unapoanza mwaka mpya 2022 warudi kivingine.

“Wasanii wenzangu, mashabiki wetu kama itawapendeza basi naomba tumalizane na haya ya amapiano kwa hii miezi miwili

iliyobaki, tunawaachia kwa mara ya mwisho mpaka Desemba 31, mwaka huu,” alisema.

Nyota huyo ambaye amekuwa akiimba nyimbo za kiharakati alisema wakianza Januari 2022 ni vema wakaanza na staili mpya nyingine au kama itafaa basi waibukie kwenye singeli.

Amapiano ni staili iliyochukua nafasi ndani ya mwaka huu asili yake ikiwa nchini Afrika Kusini lakini imeonekana
kupendwa na mashabiki wengi kutokana na aina yake ya uchezaji na uimbaji kuwa- vutia wengi.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/f0f3749310f67451a8afe5139658383c.jpeg

NCHINI Tanzania kuna matajiri wengi wakubwa walioanzia ngazi ...

foto
Mwandishi: Na Grace Mkojera

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi