loader
Stanbicyatajwabenki bora ya uwekezaji nchin

Stanbicyatajwabenki bora ya uwekezaji nchin

BENKI ya Stanbic Tanzania imetajwa kuwa Benki Bora ya Uwekezaji nchini kwa mwaka wa 2021.

Tuzo za EMEA Finance African Banking zinaangazia benki bora zaidi za kibiashara na uwekezaji katika bara zima la Afrika, ikiwa ni pamoja na mawakala na wasimamizi wa amana za uwekezaji.

Akizungumzia tuzo hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Stanbic Tanzania, Kevin Wingfield, aliwashukuru wateja wa benki hiyo akisema tuzo hiyo ni matokeo ya juhudi za pamoja kati ya wateja na washirika wengine.

Alisema vipaumbele vya kimkakati vya benki hiyo ni kukuza ukuaji endelevu na thamani nchini, kwa kutoa huduma za uwekezaji na hu- duma nyingine za benki zinazowezesha miradi muhimu kutekelezwa.

“2021 umekuwa mwaka wa mabadiliko ka- tika sekta ya benki, wakati ambapo uchumi wa dunia ukiendelea kuimarika kutokana na athari za janga linaloendelea la Covid-19,” alisema.

Aliongeza: “Tuzo hii ni uthibitisho wa kina cha utaalamu ambao tunatoa katika huduma za kibenki za uwekezaji nchini na Bara la Afrika. Tunawashukuru wateja wetu kwa kutuamini kuwahudumia.”

Mkuu wa Kitengo cha Uwekezaji wa benki hiyo, Elibariki Ndossi, alisema ushindi wa tuzo hiyo unathibitisha uongozi bora katika uwekeza- ji na ukakamavu wa benki hiyo katika kukabili- ana na changamoto.

“Kwa miaka mingi, tumejenga uwezo dhabiti wa ushauri wa uwekezaji na mikopo ndani
ya nchi, na kutoa ufumbuzi kukidhi mahitaji maalumu kwa wateja wetu na kutoa huduma nyingi za kibenki za uwekezaji kote nchini,” alisema Ndossi.

Benki ya Stanbic imeshirikiana na wateja kati- ka miradi kadhaa ya maendeleo ikiwa ni pamoja na sekta za miundombinu, nishati, mafuta na gesi, viwanda, ujenzi, na miradi ya biashara.

Benki inaamini kuwa ufadhili wa maende- leo ni kichocheo cha ukuaji wa uchumi na ni ufunguo wa kufikia malengo ya Tanzania ya viwanda.

Zaidi ya benki 200 katika bara zima zilishiriki katika tuzo za mwaka huu za EMEA Finance African Banking na Benki ya Stanbic ilishinda katika kitengo cha benki za uwekezaji.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/643265e2e915678dd8c6a2c132e1feb8.jpeg

WATANZANIA wametakiwa kuchangamkia fursa ...

foto
Mwandishi: NA MWANDISHI WETU

1 Comments

  • avatar
    Fredrick Daudi
    12/11/2021

    Hongera sana Stanbic bank

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi