loader
China, Tanzania kushirikiana kwa karibu zaidi kwa manufaa ya wote

China, Tanzania kushirikiana kwa karibu zaidi kwa manufaa ya wote

JUKWAA la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) linaendelea kukuza ukuaji wa ushirikiano wa China na Tanzania kwa kina na kiuchumi.

Tanzania kwa muda wote imekuwa ikishiriki kikamilifu katika shughuli za FOCAC, kusaidia ujenzi na maendeleo ya jukwaa hilo.

Katika miaka 21 iliyopita, China na Tanzania zimedumisha mawasiliano ya kimkakati ndani ya mfumo wa FOCAC, kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana, na kuhimiza utekelezaji wa matokeo ya mikutano yote ya awali ya FOCAC nchini Tanzania, hivyo kuleta msukumo thabiti katika maendeleo ya pamoja ya China na Tanzania.

Kutokana na ushirikiano huu, kiwango cha biashara kati ya China na Tanzania kimeongezeka kwa karibu mara 50 kutoka chini ya Dola za Marekani milioni 100 mwaka 2000 hadi Dola bilioni 4.6 mwaka jana.

Pia uwekezaji wa kampuni za China hapa Tanzania umevuka Dola za Marekani bilioni saba, huku kukiwa na miradi zaidi ya 700 ya uwekezaji na China imekuwa mshirika mkubwa wa kibiashara wa Tanzania na chanzo kikubwa cha uwekezaji wa kigeni kwa miaka kadhaa mfululizo.

Kwa mfano, Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyojengwa kwa msaada wa China, ni miradi ya kielelezo cha urafiki kati ya China na Tanzania.

Mfano mwingine ni miradi ya miundombinu inayotekelezwa na kampuni za China kama vile sehemu ya tano ya ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), upanuzi na ukarabati wa Bandari ya Dar es Salaam, miradi ya ushirikiano wa uwezo wa uzalishaji kati ya China na Tanzania kama vile ununuzi wa Maweni Limestone Ltd na Huaxin Cement, zinaendelea kwa kasi.

Aidha, China inaunga mkono kwa dhati juhudi za serikali ya Tanzania katika kupambana dhidi ya janga la Covid-19 kwa kutoa jumla ya dozi milioni 3.5 za chanjo kwa Tanzania.

Katika kipindi hiki cha kukabiliana na mabadiliko ya kimataifa na janga la Covid-19, umuhimu wa mshikamano na ushirikiano kati ya China na Afrika umekuwa dhahiri zaidi kwa kuzingatia kanuni za unyoofu na urafiki, usawa na kuheshimiana, ufanisi na utendakazi, kunufaishana na kupata matokeo ya ushindi wa pamoja.

Kwa kuzingatia umuhimu huo, Mkutano ujao wa Nane wa Mawaziri wa FOCAC utajenga maelewano mapya na kuleta msukumo mpya kwa maendeleo ya pamoja ya China na Afrika.

Mkutano huo wa Nane utafanyika mjini Dakar, Senegal Novemba 29 na 30 mwaka huu.

Hivyo, China iko tayari kufanya mawasiliano ya karibu na Tanzania na kufanya kazi na Tanzania ili kuleta manufaa zaidi ya ushirikiano ndani ya mifumo ya mpango wa ukanda mmoja, njia moja (BRI) na FOCAC, na kuimarisha ushirikiano wa kina wa ushirika kati ya China na Tanzania kwenye hatua mpya.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/ed068fd215ee46d01070bb7358e1f504.jpg

UCHUMI na maendeleo ni mambo yanayohitaji kujengewa miundombinu ...

foto
Mwandishi: Chen Mingjian, Balozi wa China Tanzania

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi