loader
Mabeyo ataja   aliyofanya Samia JWTZ

Mabeyo ataja  aliyofanya Samia JWTZ

MKUU wa Majeshi, Jenerali Venance Mabeyo amesema tangu Rais Samia Suluhu Hassan aapishwe kuwa Rais wa Tanzania Machi 19, mwaka huu, amefanya makubwa katika Jeshi la Ulinzi na Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Alisema hayo jana Dar es Salaam na kumshukuru Rais Samia kwa kulipenda jeshi hilo. 

Alisema hayo wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Mkuu wa Majeshi na Makamanda wa JWTZ cha mwaka 2021.

Jenerali Mabeyo alisema Rais Samia tangu alipoapishwa ameidhinisha kupandishwa vyeo kwa maofisa na askari wa JWTZ waliokuwa na sifa za kupandishwa vyeo.

“Umeendelea kuliamini jeshi lako kwa kuwateua maofisa na askari kushika nyadhifa mbalimbali serikalini kama vile mabalozi, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na idara na taasisi mbalimbali za serikali,” alisema.

Pia alisema walimuomba Rais Samia Sh bilioni 15 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa huko Kikombo jijini Dodoma na aliridhia. 

Alisema ujenzi huo unaendelea na akamuomba Rais Samia atembelee ili kuona maendeleo ya ujenzi huo unaotekelezwa na maofisa na askari JWTZ.

Kwa mujibu wa Jenerali Mabeyo, Rais Samia pia amelipatia jeshi hilo Sh bilioni saba kwa ajili ya kununulia sare za maofisa na askari na pia aliridhia na kuzindua Kituo cha Magonjwa Ambukizi katika Hospitali ya Jeshi Lugalo.

Alisema Samia pia aliridhia kuzindua jengo la utawala la Chuo cha Ulinzi wa Taifa lilipo Kunduchi, Dar es Salaam na kuongeza kuwa jeshi hilo liliwasilisha ombi la ajira mpya kwa lengo la kuziba mapungufu ya ikama ambalo Rais Samia pia aliliridhia.

“Umeridhia maombi yetu ya wewe kutunuku kamisheni kwa maofisa wanafunzi wanaohitimu mafunzo yao ya uofisa mwanafunzi kwa wakati jambo ambalo linaleta faraja kwa maofisa na wanafunzi hao badala ya kusubiri muda mrefu baada ya kuhitimu,” alisema Jenerali Mabeyo.

Alisema hata walipofikwa na maafa yakiwamo ya kuwapoteza askari wenzao waliokuwa katika utekelezaji wa majukumu ya kioperesheni, Rais Samia aliwatumia salamu za rambirambi jambo ambalo limeleta faraja kwa maofisa, askari na watumishi wa umma na familia zao.

Kwa upande wake, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Stergomena Taxalimweleza Rais Samia kuwa JWTZ liko imara, makamanda na askari wana ari na imani kubwa kwake.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/6d640eea7524c22bd78af0c7025868b1.jpg

JESHI la Polisi Mkoa wa Mara linamshikilia Michael ...

foto
Mwandishi: Matern Kayera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi