loader
Wawili wafa milipuko Uganda

Wawili wafa milipuko Uganda

MSEMAJI wa Jeshi la Polisi nchini Uganda, Fred Enanga amesema watu wawili waliokuwa wamebeba mabomu na kujilipua mji mkuu wa nchi hiyo, Kampala wamekufa papo hapo muda mchache baada ya kujilipua na kujeruhi raia na askari wa jeshi hilo.

Milipuko miwili imetikisa mji mkuu wa Uganda Kampala mapema siku ya Jumanne, mmoja ukiwa mita kadhaa kutoka lango kuu la kuingia katika bunge la nchi hiyo na mwingine karibu na kituo kikuu cha polisi cha mji huo.

Magari kadhaa karibu na maeneo ya milipuko yaliungua katika milipuko hiyo, huku vikosi vya uokozi, mabomu, na mashirika kadhaa ya usalama yakifanya kazi kulinda maeneo hayo.

Akiongea na Waandishi wa Habari, Enanga amesema picha za CCTV zinaonyesha wazi jinsi mtu mzima wa kiume, aliyevalia koti jeusi, na kubeba begi la nyuma, alivyojilipua. “Alikufa papo hapo na athari hiyo ilisababisha majeraha ya ziada kwa maafisa wa polisi na raia wengine ambao walikuwa ndani ya umbali wa mita 30.”

Amesema washambuliaji wawili wa kujitoa mhanga walionekana wakiwa kwenye pikipiki, wakijifanya waendesha bodaboda. Walilipua mabomu waliyokuwa wameyabeba na kuwaua papo hapo.

Mashambulizi hayo yanakuja siku 22 baada ya shambulio la bomu la kujitoa muhanga kwenye Basi la Swift Safaris. Jeshi la Polisi limedai Kikundi cha waasi wa Kiislamu nchini humo ADF kimeonesha nia ya kufanya mashambulizi mabaya, kwa malengo laini, na washambuliaji wa kujitoa mhanga na vifaa vya milipuko vilivyoboreshwa.

Polisi imesema vifaa vya kutengeneza mabomu nchini humo vinapatikana maeneo mengi ikiwa ni pamoja na maduka makubwa, masoko na maduka ya rejareja.

Hiajafahamika idadi ya majeruhi lakini magari ya kubebea wagonjwa yameonekana yakiingia na kutoka katika eneo la tukio.

Takriban mabomu manne yalilipuka katika maeneo tofauti nchini Uganda katika muda wa wiki mbili zilizopita.

Kundi la kigaidi la Daesh, pia linajulikana kama ISIS, lilidai kuhusika na moja ya mashambulizi, ingawa Rais Yoweri Museveni amesema kundi la waasi la Allied Democratic Forces (ADF) ndilo lililohusika.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/3d0a2af829741d01e7250e2e2eb77df9.png

RAIA wa Kenya wamepiga kura kwa amani na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi