loader
Wafungwa wa ugaidi waliotoroka Gereza la Kamiti Kenya wakamatwa

Wafungwa wa ugaidi waliotoroka Gereza la Kamiti Kenya wakamatwa

Wafungwa watatu wa ugaidi waliotoroka katika gereza Kuu na lenye ulinzi mkali la Kamiti, Jumatatu asubuhi, wamekamatwa.

Kwa mujibu wa Citizen Digital ya Kenya, Musharaf Abdalla almaarufu Alex Shikanda (34), Joseph Juma Odhiambo (30) na Mohammed Ali Abikar (35), wamekamatwa leo katika Msitu wa Enzio, Mwingi Mashariki, Kaunti ya Kitui nchini humo.

Aidha, wafungwa hao wamekamatwa baada ya umma kutoa taarifa, na inaaminika kuwa walikuwa wakielekea nchini Somalia.

Ripoti imeeleza kuwa magaidi hao wamerudishwa mjini Nairobi.

Ilielezwa kuwa watt hao walitoroka kwenye gereza hilo baada ya kuondoa tofali kwenye ukuta wa selo yao, kisha kutumia blanketi, nyuzi na vijiti vya ufagio kuunda kamba, na kuzitumia kuruka kuta mbili za juu kuzunguka kituo hicho.

Utorokaji huo wa kiujasiri ulipelekea maafisa kadhaa wa gereza la Kamiti kukamatwa kwa madai ya kuwasaidia wahalifu hao kutoroka.

Jana Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, alimwagiza Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Fred Matiang’i, kuhakikisha magaidi hao wanasakwa na kukakamatwa.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/70c78b74591539823773ac085a20a687.jpeg

UGANDA imekubali kuongeza maradufu idadi ya ...

foto
Mwandishi: Citizen, Kenya

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi