loader
Ayoub Lyanga mambo safi

Ayoub Lyanga mambo safi

WINGA wa Azam, Ayoub Lyanga ametoka hospitali baada ya matibabu na sasa anasubiri ripoti na programu maalumu ya jinsi ya kupona haraka jeraha lake na kurejea uwanjani. Lyanga alipata majeraha ya pua wakati akiwania mpira kwenye mechi yao dhidi ya Geita Gold walioshinda kwa bao 1-0 akapelekwa kutibiwa Afrika Kusini.

Akizungumza na HabariLEO, Ofisa Habari wa timu hiyo, Thabit Zakaria alisema matibabu ya mchezaji huyo yamefanikiwa pia ametoka wodini na anendelea vizuri na sasa inasubiriwa ripoti yake na program atakazorudi nazo kwa ajili ya kuendelea kupona majeraha yake.

“Ameruhusiwa na anaendelea vizuri kwa sasa kinachosubiriwa ni ripoti pamoja na program nyingine atakazopewa kwa ajili ya kuendelea kupona taratibu,” alisema Thabit. Mbali na Lyanga, Thabit alieleza mshambuliaji wao Prince Dube anaendelea vizuri na ameanza mazoezi baada ya kukosekana uwanjani tangu Mei, 26 mwaka huu alipoumia wakivaana dhidi ya Rhino Rangers kwenye mchezo wa Kombe la FA (Azam Sports Federation Cup).

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/66940456ab87d6f1ffcac125b547e718.jpeg

MAKOCHA wa Simba Pablo Franco na wa Yanga, ...

foto
Mwandishi: Na Hans Mloli

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi