loader
Profesa Jay ‘apiga dongo’ Basata

Profesa Jay ‘apiga dongo’ Basata

MSANII wa Bongo Fleva, Joseph Haule ‘Profesa Jay’, amesema anashangaa kwanini Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) wanakuwa wakali kwenye nyimbo za siasa na siyo zile zinazoimba lugha isiyo nzuri yenye kuzungumzia zaidi mapenzi.

Akizungumza Dar es Salaam Profesa Jay alisema kuna baadhi ya nyimbo za mapenzi zinazoimbwa siku hizi huwezi kuzisikiliza ukiwa na watoto.

“Nashangaa Basata wanakuwa wakali kwenye mambo ya siasa lakini kwenye mapenzi wakija kusikiliza na kuchambua lugha ni ngumu huwezi kusikiliza lakini wasanii wanakuambia wanafanya vile sababu ni biashara na watu wanapenda, lazima kuwe na uwiano ili kutengeneza kizazi chenye nidhamu kama sisi,” alisema Profesa Jay.

Pia aliwapongeza wasanii wa Kenya kwa harakati zao za kupinga wasanii wa nje kulipwa zaidi kuliko wasanii wazawa na kutaka mamlaka kutengeneza sheria ambazo zitasaidia kukuza vipaji kutoka Tanzania. “Kwanza niwapongeze wasanii wa Kenya kwa kupata mwamko huo.

Kwa mfano sasa Tanzania kwenye maeneo mbalimbali ya starehe wanamuziki kutoka nchini Afrika Kusini wamechukua nafasi kubwa kiasi kwamba nyimbo za ndani hazizingatiwi,” alisema Profesa Jay.

“Wakati huo tunacheza ngoma Afrika Kusini wenyewe wana ile sheria ambayo imepitishwa kusimamia maudhui ya ndani kwa asilimia 85-90 halafu muziki mwingine kutoka maeneo mengine uchezwe kwa asilimia zilizobaki,” alisema.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/1c3b200a162def9366451c7e0fc7798a.jpeg

NCHINI Tanzania kuna matajiri wengi wakubwa walioanzia ngazi ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi