loader
Dstv Habarileo  Mobile
Aomba Mkoa wa Katavi  uungwe na gridi ya taifa

Aomba Mkoa wa Katavi uungwe na gridi ya taifa

MKUU wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko ameiomba serikali iharakishe utekelezaji kuunga mkoa huo kwenye umeme wa gridi ya taifa ili kupunguza gharama za kutumia umeme wa mafuta.

Mrindoko alitoa ombi hilo kupitia kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo ambaye alifika mkoani humo kwa ziara ya siku mbili kukagua utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya chama hicho na kuhimiza uhai wa chama ngazi ya mashina.

Alisema ukosefu wa umeme wa gridi katika mkoa huo unasababisha kuwepo kasi ndogo ya uanzishwaji wa viwanda na pia gharama za uendeshaji ni kubwa.

Kaimu Meneja wa Shirika la Umeme wa mkoa huo, Godfrey Josephat alisema gharama za uzalishaji wa umeme wa mafuta ni kubwa na kwamba, na sasa inafikia shilingi milioni 37 hadi 43 kwa siku, sawa na shilingi bilioni moja hadi bilioni 1.3 kwa mwezi.

Josephat alisema makusanyo ya shirika mkoani humo kwa mwezi ni kati ya shilingi milioni 500 hadi 668. Alisema kwa sasa umeme unaofuliwa ni megawati 5.816. Alisema kuna mahitaji ya megawati 9.5 kutoka kwa viwanda vya Katavi Mining ambacho kinahitaji umeme wa megawati 8.0, kiwanda cha maji na nafaka 0.5, kiwanda za madini cha Mlele megawati 0.5, mgodi wa Kapalamsenge megawati 0.5.

Alisema serikali Kwa kushirikiana na Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) umeanza kutekeleza mpango wa kufikisha gridi ya Taifa katika mkoa huo wa Katavi kwa gharama za shilingi bilioni 64.9. Josephat alisema Tanesco imeshakamlisha ujenzi wa vituo vya kupokea na kupoza umeme kutoka Ipole, Inyonha na Mpanda mkoani Katavi.

“Kazi ya ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Tabora mpaka Mpanda wa Kilovoti 132 upo katika hatua ya utekelezaji ambapo kazi za kusafirisha njia imefikia kilomita 179 Kati ya kilomita 383 Sawa na asilimia 46.7”alisema.

Josephat alisema nguzo zilizosambazwa ni 520 kati ya 4,090 sawa na asilimia 12.71 na uchimbaji wa mashimo 246 kati ya 490. Chongolo alisema ni muhimu mkoa huo uunganishwe kwenye gridi ya taifa kwa kuwa Tanesco mkoani humo inajiendesha kwa hasara.

“TANESCO hapa haijiendeshi kwa faida, inajiendesha kwa hasara kwa sababu matumizi yanazidi mapato yanayokusanywa, ili kuepusha kupata hasara kwa shirika inabidi serikali kupitia wizara ya nishati ifanye haraka kuleta umeme wa gridi ili kusaidia shirika kujiendesha kwa faida na kumpunguzia mwanachi gharama,”alisema.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/68856f5ce5189b1202fd7cc42132951b.jpg

SERIKALI imepanga kujenga ...

foto
Mwandishi: ANNE ROBI

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi