loader
Dstv Habarileo  Mobile
NEMC yataka  halmashauri  kuzingatia sheria  za mazingira

NEMC yataka halmashauri kuzingatia sheria za mazingira

BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limezitaka halmashauri zote zisimamie sheria za utunzaji mazingira kwa lengo la kuepusha athari zitokanano na uharibifu wa mazingira.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Baraza hilo, Dk Samuel Gwamaka (pichani) alisema ukosefu wa mvua unaojitokeza katika maeneo mengi nchini kwa sasa kwa kiasi fulani inatokana na matokeo ya uharibifu huo na kuitaka jamii kubadilika.

Dk Gwamaka alisema kwa uchunguzi walioufanya katika maeneo mengi nchini wamebaini kuwa maeneo mengi oevu na yenye vyanzo vya maji yameingiliwa na shughuli nyingi za kibinadamu zikiwemo za ujenzi hali inayosababisha maji katika mito kupungua.

“Katika kutatua changamoto hiyo sisi kama taasisi ya Serikali tuliopewa jukumu la kusimamia mazingira tayari tumeshachukua hatua mbalimbali za kulinda mazingira hayo mojawapo ni pamoja na kuhakikisha tunasimamia kikamilifu sheria zilizopo” alisema Dkt Gwamaka 

Aidha aliisisitiza kwa kuzitaka taasisi zote za Serikali hususani Halmashauri za majiji, miji manispaa pamoja na wilaya kuendelea kushirikiana na baraza hilo kusimamia sheria hizo ili pamoja na mambo mengine waweze kulimaliza tatizo la uharibifu wa mazingira.

Alisema kama halmashauri hizo pamoja na zile za vijiji zingekuwa zinasimamia vizuri sheria na sera inazozitunga kwa kiasi kikubwa changamoto ya uharibifu wa mazingira inayojitokeza katika maeneo mengi isingeitokeza.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/06859517fd974ef927e38275a2f9243a.png

SERIKALI imepanga kujenga ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi