loader
Mganda avunja rekodi ya Dunia Lisbon

Mganda avunja rekodi ya Dunia Lisbon

MGANDA Jacob Kiplimo amevunja rekodi ya dunia katika mbio za nusu marathoni za Lisbon zilizofanyika juzi, akitumia muda wa dakika 57:31 katika mbio inayotambulika na Shirikisho la Kimataifa la Riadha, WA.

Bingwa huyo wa dunia wa nusu marathoni alishinda mbio hizo kwa zaidi ya sekunde moja akiipita rekodi iliyopita iliyowekwa na Mkenya, Kibiwott Kandie huko Valencia, Hispania mwaka jana.

Kiplimo, aliyemaliza wa tatu katika mbio za meta 10,000 na watano katika meta 5,000 katika Michezo ya Olimpiki iliyofanyika Tokyo hivi karibuni alipita katika kilometa tano akitumia dakika 13:40.

Wakati akifika kilometa 10 alikuwa ametumia dakika 27:05, akiwa anaongoza kwa takribani dakika moja na tayari alikuwa mbio kuvunja rekodi ya dunia ya Kandie.

Kiplimo alimaliza kilometa 15 kwa kutumia dakika 40:27, ikiwa ni muda wa kasi zaidi kwa umbali huo na kumaliza ndani ya dakika 57.

Mwanariadha huyo alimaliza mbio hizo kwa kutumia dakika 57:31 na kuweka rekodi ya dunia.

Muethiopia Esa Huseyidin Mohamed alimaliza wa pili kwa kutumia dakika 59:39, ikiwa ni mbele ya Muethiopia mwenzake, Gerba Beyata Dibaba, ambaye alimaliza kwa muda kama huo katika nafasi ya tatu. 

Wachezaji wote tisa kwa upande wa wanaume walimaliza ndani ya dakika 60.

Kwa upande wa wanawake, Muethiopia  Tsehay Gemechu alishinda kwa kutumia saa 1:06:06 huku Mkenya Daisy Cherotich (alitumia 1:06:15) na Joyce Chepkemoi (1:06:19).

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/d9c54feae48e2a88d4ef0ff9d83db1cd.jpeg

RAIA wa Kenya wamepiga kura kwa amani na ...

foto
Mwandishi: KAMPALA, Uganda

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi