loader
Ushirikiano Serikali na wananchi ujenzi wa madarasa waokoa bil 197/-

Ushirikiano Serikali na wananchi ujenzi wa madarasa waokoa bil 197/-

Zoezi la uchimbaji msingi katika ujenzi wa vyumba vya madarasa mkoani Mwanza, lililofanyika kwa ushirikiano wa Serikali na wananchi, limefanikiwa kuokoa Sh milioni 197 ambapo fedha hizo zitatumika kufanya shughuli nyingine ikiwemo kutatua kero za elimu hususan ukosefu wa nyumba za walimu.

Akizungumza wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Robert Gabriel, amewasisitiza viongozi wa wilaya kuongeza kasi ya ujenzi na kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za Serikali.

RC Gabriel pia amemtaka Mkurugenzi  wa Buchosa kutatua kero ya upatikanaji wa saruji katika maeneo ujenzi unapoendelea, ili kusiwepo na sababu yoyote ile ya kuchelewesha miradi kukamilika.

Ujenzi wa madarasa unatazamiwa kukamilika Desemba 15 mwaka huu, ili kuanza kuwapokea wanafunzi wapya watakaojiunga, na wale watakao endelea na masomo mwakani.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/a7f58830f23b1fed3240194c984b9bfd.jpeg

JESHI la Polisi Mkoa wa Mara linamshikilia Michael ...

foto
Mwandishi: Anthon Chuwa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi