loader
Prof Mkumbo: Tanzania kuna uhuru wa kutosha biashara na uwekezaji

Prof Mkumbo: Tanzania kuna uhuru wa kutosha biashara na uwekezaji

Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof Kitila Mkumbo, amewahakikishia wawekezaji na wafanyabiashara kuwa Tanzania kuna uhuru wa kutosha wa kufanya biashara na uwekezaji, na kuwa Serikali itaendelea kutekeleza wajibu wake kikamilifu ikiwemo kuweka mazingira mazuri ya sera na  sheria.

Akizungumza jana alipomuwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika hafla ya kuadhimisha miaka 60 ya kuanzishwa kwa Kiwanda cha Sigara (TCC), jijini Dar es Salaam, Prof Mkumbo alisema yote hayo ni kuhakikisha wanafa biashara katika utulivu na  kupata faida hatimaye Serikali iweze kufaidika kupitia ajira kwa wananchi na kupata kodi.

“Tunatambua kwamba  ili uchumi wetu uendelee kukua na kufikia malengo tuliyojiwekea katika mpango wa tatu wa maendeleo wa miaka mitano 2021/22 – 2025/ 26, tunahitaji uwekezaji uliopo nchini uendelee kufanya kazi vizuri kwa utulivu lakini pia tupate uwekezaji mpya,” alisema Prof Kitila Mkumbo.

Aidha, alisema kuwa Tanzania kuna utulivu wa siasa na amani ya kutosha ambapo ni kigezo cha kwanza kwa wawekezaji wote duniani, na pia Serikali itaendelea kuwekeza katika miundombinu mbalimbali ya kuwezesha uzalishaji  viwandani, kama barabarabara na maji ikiwemo kufanyia kazi na kumaliza changamoto ya umeme kupitia miradi mbalimbali inayokutekelezwa nchini.

Prof Mkumbo ametoa wito kwa wenye viwanda na wawekezaji, kuhakikisha wanazingatia kikamilifu sheria na kanuni zinazoongoza sekta ya viwanda hapa nchini ikiwemo kuheshimu sheria zinazohusu kazi, ili watumishi wanaoajiriwa wafanye kazi katika mazingira mazuri na kulipwa ujira sitahiki kwa mujibu wa sheria.

Mbali na hayo, ametoa rai kwa makampuni na wafanyabiashara wa Tanzania kujikita katika ushindani katika kipindi hiki ambacho Tanzania imejiunga katika mkataba wa eneo huru la biashara (AfCFTA), wenye nchi wanachama 54.

Kwa upande wake Naibu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi, ameipongeza kampuni ya TCC kwa kuweza kutoa ajira za moja kwa moja zaidi ya 418, na ajira nyingine zisizo za kudumu.  Pia ameipongeza kwa kuendelea kutoa fedha kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, itakayowasaidia wafanyakazi, ili pale watakapomaliza kazi wapate pesa za kuwasaidia katika kipindi ambacho hawapo kazini.

Nae Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya TCC, Michal Bachan, alisema kuwa wanajivunia kwa kipindi cha miaka 60 ya kuanzishwa kwa kampuni hiyo, na kuwa ni safari yenye mafanikio ambayo imeisaidia kuwa na mchango mkubwa katika pato la Serikali ambalo limeongezeka kufika wastani wa bilioni 220.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/e58fbe938046f58aad145128a55feb04.jpeg

JESHI la Polisi Mkoa wa Mara linamshikilia Michael ...

foto
Mwandishi: Iddy Mwema

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi