loader
Waliopata ujauzito shuleni ruksa kuendelea - Profesa Ndalichako

Waliopata ujauzito shuleni ruksa kuendelea - Profesa Ndalichako

SERIKALI imeondoa vikwazo kwa kutoa fursa kuendelea na masomo kwa wanafunzi waliokatiza masomo kwa sababu mbalimbali wakiwamo wasichana ambao wanapata ujauzito wakiwa katika shule za msingi au sekondari.

Hatua hiyo inaruhusi wanafunzi kuendelea na masomo yao katika mfumo rasmi baada ya kujifungua.

Haya yamebainishwa jana jijini hapa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako wakati wa kuelezea  mwelekeo katika sekta ya elimu.

“ Wanafunzi waliokatiza masomo yao kwa sababu mbalimbali watapewa fursa ya kurejea shuleni, fursa hizo zitajumuisha wasichana ambao wanapata ujauzito wakiwa katika shule za msingi au sekondari.”

“ Wanafunzi hao wataruhusiwa kuendelea na masomo yao katika mfumo rasmi baada ya kujifungua.”

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/ca4e5010dfb985d181f5898d70f9c7e3.jpg

JESHI la Polisi Mkoa wa Mara linamshikilia Michael ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi