loader
Makala: Hali si nzuri mgao wa Maji upo sana, upungufu Lita ml.70

Makala: Hali si nzuri mgao wa Maji upo sana, upungufu Lita ml.70

MGAO wa Maji jijini Dar es Salaam kuendelea kuwepo kwa muda mrefu kutokana na kuwa na upungufu wa Lita milioni 70.

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala ambae leo pamoja na Kamati nzima ya usalama ya mkoa wametembelea kukagua mitambo ya kuzalisha maji ya Ruvu juu na Ruvu chini.

Makala amesema kwa uzoefu wake akiwa Naibu Waziri wa Maji, uzalishaji wa Maji ni  lita milioni 520 ambazo ndizo zinatosheleza kwa Jiji la Dar es Salaam ambapo vyanzo vikuu ni kutoka Ruvu Juu na Ruvu chini.

Amesema wakati  maelekezo yaliyotolewa na Rais Samia Suluhu na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa yanatoka, kulikuwa na uzalishaji wa lita 65 lakini baada ya kudhibiti wavamizi imesaidia kuongezeka kwa  lita milioni 200 na kufanya kuwa na upungufu wa lita milioni 70 kwa Ruvu chini.

Kwa upande wa  upande wa Ruvu juu hali sio mbaya sana kutokana na uzalishaji wa maji kuendelea kuwa lita milioni 196 kwa siku.

"Baada ya kudhibiti wavamizi kwenye vyanzo vya maji kwa sasa maji yanayozalishwa ni lita milioni 200 bado hali sio nzuri, mgao wa Maji utaendelea kuwepo kwa muda mrefu tukisubiri kudra za Mwenyenzi Mungu mvua inyeshe , tulitegemea mvua za vuli lakii kukosekana kwa mvua hizo kwa takribani miezi miwili sasa imesababisha upungufu mkubwa na hali ikiwa hivi sijui itakuwaje, wananchi ingieni kwenye maombi" amesema Makala na kuongeza

"Kina kinazidi kushuka, kama ya kibinadamu tumefanya kwa kadri ya uwezo wetu, sasa tunategemea kudra za Mwenyenzi Mungu, kila mmoja kwa imani yake aombee mvua, hali ni mbaya, ni lazima tuseme ukweli, Mameya, Wakuu wa Wilaya kawambieni wananchi wenu ukweli, msifiche fiche hali ni mbaya," amesisitiza Makalla.

Aidha  kutokana ana hali hiyo, ametoa wito kwa Wananchi kutumia Maji vizuri na kuendelea kutunza vyanzo vya maji huku akipongeza jitiada zinazofanywa na na Dawasa.

Nae Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar Es salam na Pwani (DAWASA), Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema watajitaidi kadri inavyowezekana kupambana na upungufu wa Maji.

Amesema kina cha maji cha mto Ruvu kimepungua kufuatia kiangazi cha muda mrefu

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/08eab2bbda27a59ff263172cfc672957.jpg

JESHI la Polisi Mkoa wa Mara linamshikilia Michael ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi