loader
Kurejea safari za ATCL Kenya kuimarisha biashara

Kurejea safari za ATCL Kenya kuimarisha biashara

RAIS Samia Suluhu Hassan ameipongeza Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) kwa kupanua huduma za safari ndani na nje ya nchi ikiwemo kurejesha safari za Dar es Salaam – Nairobi nchini Kenya zitakazoanza kesho.

Rais Samia amewaomba Watanzania waiunge mkono ATCL ili izidi kukua zaidi.

“Ni matarajio yangu kuwa tutaendelea kuiunga mkono ATCL ili ikue zaidi na kutimiza matarajio ya Watanzania,” alisema Rais Samia katika ujumbe alioandika kwenye ukurasa wake katika mtandao wa kijamii wa Twitter.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa ATCL, Josephat Kagirwa alisema safari za ATCL kwenda Nairobi zitakuwa zikifanyika mara mbili kila siku.

Kagirwa alisema kutakuwa na ndege itakayoondoka Dar es Salaam asubuhi kwenda Nairobi na kurudi na nyingine itaondoka jioni na kurudi.

Alisema nauli zao ni nafuu kwa kuwa safari moja tu ya kwenda ni Dola za Marekani 210 (takriban Sh 480,000). Alisema kwa kuanzia ndege itakayokuwa inatumika kwa safari hizo ni Airbus A220-300 na nyingine zinaweza kutumika kulingana na wingi wa abiria.

“Tutaanza safari za Nairobi mara mbili kwa siku, asubuhi na jioni ili kuwawezesha watu walioko Tanzania kufanya shughuli zao Nairobi na kurudi au walioko Nairobi kuja hapa kufanya shughuli zao na kurudi, wasiopenda kulala waweze kufanya hivyo,” alisema Kagirwa.

Kagirwa alisema safari hizo kiuchumi zina umuhimu kwa kuwa Tanzania na Kenya zinashirikiana kiuchumi kwa sababu bidhaa za kila nchi zinapatikana upande wa pili na wafanyabiashara wa nchi hizo wanatembelea masoko ya nchi zote mbili.

Alisema safari hizo zitaongeza wigo kwa Watanzania na Wakenya kufanya biashara kwa pamoja na kwa haraka na kwa utalii itakuwa rahisi kwa watalii wanaofika Kenya kuja kutembelea vivutio vya Tanzania.

Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama na Uwezeshaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Zacky Mbene alisema safari hizo ni muhimu kwa usafiri na usafirishaji kwa kuwa Nairobi imekuwa kitovu cha biashara kwa Afrika Mashariki.

Mbene alisema kwa kuwa jitihada za Tanzania ni kulifikia soko la Kenya, kwa sasa Tanzania inafanya vizuri kwenye bidhaa za chakula, kilimo na kidogo kwenye bidhaa za viwandani zikiwemo marumaru na vioo, hivyo usafiri utaleta hamasa kwa Watanzania kushiriki katika uchumi wa Kenya.

“Kwetu sisi Watanzania ni faida, tunaona ni namna nzuri ya kuchukua soko hilo, italeta faida kwa nchi yetu na kwa sekta binafsi na ATCL itatumika kama dirisha la kutangaza vivutio vya Tanzania, kwa hiyo Watanzania tuiunge mkono ATCL,” alisema Mbene.

Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT), Stephen Chamle alisema safari hizo za ATCL kwenda Nairobi ni muhimu kiuchumi kwa kuwa biashara kati ya Tanzania na Kenya ni mazao ya kilimo yakiwemo maua na matunda.

Chamle aliiomba ATCL ianzishe safari za kwenda Dubai, Uturuki na nchi nyingine za Asia ambako wanafanya biashara nao kwa sababu bado hakuna uhuru wa kwenda China kwa sababu ya janga la Covid-19.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/773ee6369faaf5d229944db4ddc3e06b.jpeg

JESHI la Polisi Mkoa wa Mara linamshikilia Michael ...

foto
Mwandishi: Matern Kayera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi