loader
Dstv Habarileo  Mobile
TASWO YAKABILIWA NA UPUNGUFU WA MAOFISA USTAWI WA JAMII

TASWO YAKABILIWA NA UPUNGUFU WA MAOFISA USTAWI WA JAMII

CHAMA cha watalaam wa ustawi wa jamii nchini(TASWO) kimeiomba Serikali  kusaidia utatuzi wa upungufu wa maofisa ustawi wa jamii.

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa chama hicho Dk Mariana Makuu wakati wa uzinduzi wa mkutano wa siku nne. ‘’Changamoto ya upungufu wa maofisa ustawi wa jamii bado ni kubwa sana haswa katika Serikali za mitaa’’ alisema Dk Makuu.

Alisema kada ya ustawi wa jamii ina mapungufu wa watumishi zaidi ya asilimia 80 katika ngazi ya kata na asilimia 60 kwa ngazi ya wilaya. ‘’Tunaomba sana Serikali itusaidie katika ufuatiliaji wa kibali cha dharura ambacho tuliomba kwa Waziri Mkuu katika washa iliyokutanisha maofisa ustawi wa jamii wote nchini Januari 2019 mwaka huu’’ alisema Dk Makuu.

Alisema kibali hicho kikitoka kitasaidia kuajiri watumishi wa ustawi wa jamii ngazi ya Halmashauri na Maofisa ustawi wa jamii wasaidizi ngazi ya kata. Naye Waziri wa Afya Dk Dorothy Gwajima alisema Serikali inaendelea kujipanga kuona namna ambayo itaongeza kuwaajiri wataalamu wa sekta ya ustawi wa jamii.

Alisema anatoa wito kwa wadau wote kutumia mwongozo wa kitaifa wa watu wanaojitolea kusaidia kuajiri wataalam wa ustawi wa jamii katika ngazi mbalimbali ili kukidhi utoaji wa huduma.

 

Alisema Serikali imechukua hatua mbalimbali kwa lengo la kuboresha utoaji huduma za ustawi wa jamii ikiwa ni pamoja na kutoa miongozo ya huduma na kuratibu mafunzo kwa maafisa Ustawi wa Jamii waliopo Mwisho

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/df7c881d83fa89f7431519365aea4a4e.jpg

SERIKALI imepanga kujenga ...

foto
Mwandishi: Na Alexander Sanga

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi