loader
Wote waliofaulu la saba wapangwa kidato cha kwanza

Wote waliofaulu la saba wapangwa kidato cha kwanza

SERIKALI imetangaza uchaguzi kwa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2022.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Ummy Mwalimu alisema jana nafasi kwa wanafunzi wa bweni ni za shule za kitaifa.

Ummy aliwaeleza waandishi wa habari jijini Dodoma kuwa wanafunzi 907,802 waliofaulu wakiwemo wasichana 467,967 na wavulana 439,835 ambao ni sawa na asilimia 81.97 ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi mwaka huu wamechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza. 

Alisema kati ya waliofaulu na kupangiwa kujiunga na kidato cha kwanza wamo 2,673 wenye mahitaji maalumu sawa na asilimia 0.29 ambao kati yao wavulana ni 1,471 na wasichana 1,202.   

Ummy alisema kwa mwaka 2022 kumekuwa na ongezeko la wanafunzi 73,932 sawa na asilimia 8.87 ya wanafunzi waliofaulu ukilinganisha na mwaka jana ambapo wanafunzi 833,872 walifaulu na kupata sifa ya kujiunga na kidato cha kwanza. 

Alisema wanafunzi wote 907,802 waliofaulu mtihani wa darasa la saba nchini mwaka huu wataanza masomo siku moja.

“Hivyo natumia fursa hii kutangaza kuwa muhula wa masomo kwa shule za msingi na sekondari zinazomilikiwa na serikali kwa mwaka 2022 utaanza tarehe 17 Januari 2022,"alisema Ummy. 

Alisema hatua ya serikali ya kutoa Sh bilioni 240 kujenga madarasa 12,000 nchi nzima imeongoza nafasi kutoka  nafasi 430,604 zinazoachwa na wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne mwaka 2021 hadi kufikia nafasi 1,030,604 pindi madarasa yanayojengwa yakikamilika yatakayoongeza nafasi 600,000.

Ummy alisema kuchagua wanafunzi wa kidato cha kwanza kumezingatia mwanafunzi kufikisha jumla ya alama za ufaulu kuanzia 121 hadi 300.  

Alisema mgawanyo wa wanafunzi kwa shule za bweni zenye ufaulu mzuri na zile za bweni ufundi zimegawanywa kwa kila mkoa kulingana na idadi ya watahiniwa waliosajiliwa katika mkoa husika kwa kutumia kanuni ya kugawa nafasi hizo kitaifa. 

Alisema kwa shule za sekondari za bweni za kitaifa za kawaida zimegawanywa kwa kila halmashauri kwa kuzingatia idadi ya watahiniwa waliotoka katika mazingira magumu kwa kutumia kanuni ya kugawa nafasi hizo kitaifa.

Ummy alisema wanafunzi 934 ikiwa wavulana 514 na wasichana 420 sawa na asilimia 0.1 wamechaguliwa kujiunga na shule za sekondari za wanafunzi wenye ufaulu mzuri zaidi.

Alisema wanafunzi 1,265, wavulana wakiwa ni 1,070 na wasichana 195 sawa na asilimia 0.14 wamechaguliwa kwenda shule za sekondari za ufundi.

Alisema wanafunzi 1,989, wavulana wakiwa ni 1,036 na wasichana 953 sawa na asilimia 0.22 wamechaguliwa kujiunga na shule za sekondari za bweni kawaida wakati wanafunzi 903,614 kati yao wavulana 437,215 na wasichana 466,399 sawa na asilimia 99.54 wamechaguliwa kujiunga na sekondari za kutwa.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/02c9cb75834129390a346fa8e5ab170f.jpeg

JESHI la Polisi Mkoa wa Mara linamshikilia Michael ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi