loader
Naibu Waziri akutana na viongozi vyama vya wafanyabiashara za utalii Rwanda

Naibu Waziri akutana na viongozi vyama vya wafanyabiashara za utalii Rwanda

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amefanya kikao na viongozi wa vyama vya wafanyabiashara za utalii nchini Rwanda kwa lengo la kujadili namna bora ya kuboresha, kukuza na kuendeleza sekta ya utalii nchini Tanzania.

Akizungumza katika kikao hicho, Naibu Waziri Mary amekubaliana na viongozi wa vyama vya wafanyabiashara za utalii nchini Rwanda kutafuta namna bora ya kuwaunganisha wadau wa utalii wa Rwanda na wa Tanzania ili kukuza utalii wa nchi zote mbili.

Katika majadiliano hayo, Naibu Waziri huyo wa Utalii amepata ufafanuzi kutoka kwa viongozi hao kuhusu namna ambavyo Serikali ya Rwanda inashirikiana na sekta binafsi katika kuendeleza utalii na mbinu ambazo Serikali hiyo inatumia kupata wawekezaji hasa katika utalii wa mikutano. 

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu, Idara ya Utalii ya Rwanda, Frank Mugisha amesema kuwa ofisi yake imekuwa ikifanya kazi na Tanzania kupitia Chama cha Mawakala wa Utalii Tanzania (TATO) ambacho hushirikiana na Serikali ya Ujerumani katika utunzaji wa Hifadhi za wanyamapori hasa kwenye Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Wafanyabiashara hao wamependekeza kwamba mwaka 2022 Serikali ya Tanzania na Rwanda iandae maonesho ya road shows kwa pamoja katika nchi za Ulaya ambako kuna wanunuzi wakubwa wa vivutio vya utalii lengo ikiwa ili kutangaza vivutio vya utalii vya nchi zote mbili kwa kauli mbiu ya “Visit Tanzania and Rwanda”

Aidha, wafanyabiashara hao wameahidi kuitembelea Tanzania mwezi Desemba mwaka huu kwa lengo la kujifunza zaidi kuhusu vivutio vya utalii na maeneo ya uwekezaji yaliyopo nchini Tanzania ili waweze kuwekeza, kuviuza vivutio hivyo na pia kuvisemea kwenye biashara zao.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/451e85f635dbc659cde1452d3d01fa50.jpeg

JESHI la Polisi Mkoa wa Mara linamshikilia Michael ...

foto
Mwandishi: Iddy Mwema

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi