loader
Wadaiwa HESLB wakumbushwa kulipa

Wadaiwa HESLB wakumbushwa kulipa

Wanufaika wa Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu wametakiwa kuhakikisha wanalipa mikopo hiyo ili wengine waweze kupata mikopo hiyo kwa wakati.

Wito huo umetolewa jijini Dodoma na Meneja wa Kanda ya Kati wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Octavian Seleman wakati wa kuelimisha wananchi kuhusu kampeni ya sifurisha iliyolenga kuhamasisha wanufaika kumaliza madeni ya mikopo hiyo.

“Sifurisha ni kampeni inayowalenga wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu ambao mikopo yao imebaki kidogo kwa ajili ya kuimaliza, mnufaika anaweza kumaliza mkopo wake kwa kulipa kwa kupitia taasisi za huduma za kifedha na kisha tunamuandikia barua.” amesema Meneja huyo.

Pia amewahamasisha wanufaika waliopo kwenye sekta isiyo rasmi nao waweze kulipa mkopo wanaodaiwa ili watu wengine waweze kunufaika na mikopo hiyo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/3eea3e09f73b06d1ad08eefefab7e5f4.png

JESHI la Polisi Mkoa wa Mara linamshikilia Michael ...

foto
Mwandishi: Iddy Mwema

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi