loader
Yanga hakuna kulala

Yanga hakuna kulala

VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga leo wataingia kambini Avic Town Kigamboni kujiandaa na mchezo unaofuata dhidi ya Mbeya Kwanza ambao utapigwa Novemba 30 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Msafara wa miamba hiyo ya soka nchini unatarajiwa kuanza safari ya kwenda Mbeya Jumapili asubuhi kwa usafiri wa ndege kwa ajili ya pambano hilo dhidi ya timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu kwa mara ya kwanza.

Ofisa Habari wa timu hiyo, Hassan Bumbuli alisema jana kuwa, wachezaji wote wataingia kambini kuanzia leo mchana Avic Town na watakuwa huko  mpaka siku ya safari ya kwenda Mbeya kwa ajili ya pambano hilo ambalo wamedhamiria kushinda ili kurudi katika wimbi la ushindi waliloanza nalo msimu huu.

Alisema tangu watoke Lindi ambako timu yao ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Namungu, wachezaji walipewa mapumziko na leo wataingia kambini rasmi kujiandaa dhidi ya Mbeya Kwanza.

Kwa upande wake Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh alisema miongoni mwa nyota watakaoingia kambini ni kiungo raia wa Uganda, Khalid Aucho aliyekosekana kwenye michezo miwili ya ligi kutokana na jeraha alilokuwa nalo kwenye goti la mguu wa kushoto.

Hafidh alisema kiungo huyo amesharejea nchini na anaendelea vyema na mazoezi na atakuwa ni miongoni mwa wachezaji watakaosafiri na timu Jumapili kwenda Mbeya kwa ajili ya pambano na Mbeya Kwanza.

Aucho ni nguzo muhimu kwenye kikosi cha vinara hao wa soka nchini kutokana na uhodari wake aliouonesha kwenye mechi kadhaa alizoichezea timu hiyo kwenye ligi na kukosekana kwake kulionesha mapungufu kiasi na kurejea kwake kumeibua furaha kwa mashabiki wenye matumaini ya kuona wanabeba taji la Ligi Kuu msimu huu.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/2517f3496049e6da99b40e43aba60f06.jpeg

MAKOCHA wa Simba Pablo Franco na wa Yanga, ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi