loader
Dstv Habarileo  Mobile
Mambo 4 yapendekezwa  kumaliza ukatili wa kijinsia

Mambo 4 yapendekezwa kumaliza ukatili wa kijinsia

SIKU 16  za kupinga ukatili wa kijinsia, wanaharakati wamependekeza mambo manne kwa serikali ili kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Mambo ni serikali kutunga sheria ya kudhibiti ukatili wa jinsia kwani ukosefu wa sheria mahususi ya makosa ya ukatili ni changamoto kubwa katika upatikanaji wa haki kwa watendewa na kuwatia hatiani watuhumiwa.

Kuharakishwa kwa mabadiliko ya sheria ya ndoa ya mwaka 1971 ili kuokoa mabinti dhidi ya ndoa za utotoni, kuboresha muundo na kutengwa bajeti ya kutosha kwa ajili ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA).

Pia na kufuta sheria zote za kibaguzi mathalani sheria ya kimila ya mirathi, tangazo la serikali namba 436 la mwaka 1963 ambayo inanyima wanawake haki yao ya kikatiba ya kumiliki mali kupitia urithi.

Mratibu Kitaifa, kutoka Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo Afrika (WiLDAF), Anna Kulaya amesema hayo leo jijini Dar es Salaam, katika katika uzinduzi wa siku 16 za uanaharakati dhidi ya ukatili wa kijinsia.

Amesema mwaka huu asasi za kiraia zinaangazia maeneo makuu manne ambayo ni ukatili majumbani, ukatili dhidi ya wenza au wapenzi, rushwa ya ngono na ukatili wa mitandaoni hasa kwa wanawake ambao wamekutana na aina mpya ya ukatili unaofanyika mitandaoni kitu ambacho kinapelekea baadhi ya wanawake kujiweka kando na mitandao

“Ikumbukwe kuwa kutokana na ugonjwa wa Corona watu wamekuwa wakitumia teknolojia ya tehama na mitandao kama sehemu ya kupata taarifa.

“Wapo pia wanaotumia mitandao kukuza biashara zao lakini kuna baadhi ya watu wanatumia hii mitandao kuwafanyia wanawake ukatili wa kijinsia,” amesema Anna.

Aidha, Anna amesema matukio ya ukatili kwa watoto yaliyoripotiwa na Jeshi la Polisi kati ya kipindi cha Januari 2021 mpaka Septamba yanaonesha kuwa watoto 6168 kati yao wasichana 5287 na wavulana 88 wamefanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Amesema kati ya hao watoto 3524 walibakwa, 637 walilawitiwa, 1887 walipata mimba na 130 walichomwa moto.

“Kinachosikitisha zaidi ni kuwa kati ya visa vilivyoripotiwa watuhumiwa waliofikishwa mahakamani ni 3,800 tu, kesi zilizofanyiwa upelelezi ni 2,368 na kesi zilizotolewa hukumu ni 88 tu.

“Takwimu hizi zinatoa taswira ya ukubwa watatizo hasa katika mifumo yetu ya kushugulikia upatikanaji wa haki, wakati sasa umefika wa kila mmoja wetu kutimiza wajibu wake katika kukomesha vitendo vya ukatili.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/c5504fddf42f74c838654027c9c44985.jpeg

SERIKALI imepanga kujenga ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi