loader
Dstv Habarileo  Mobile
Taaluma ya Meli haijatambulika – Nguhilla

Taaluma ya Meli haijatambulika – Nguhilla

MHADHIRI wa Chuo cha Bandari Julius Nguhilla amezindua katibu chake ambacho kinazungumzia masula mbali mbali ya usafirishaji kwa njia ya bandari na faida za uchumi wa buluu.

Akizunguza katika hafla ya uzinduzi wa kitabu hicho, Nguhilla amesema taaluma ya usafirishaji kwa njia ya meli haijatambulika kama zilivyo taaluma nyingine za wanasheria, madaktari na wahasibu.

“Mkurugenzi wa zamani wa CRDB Dk Charles Kimei asingeweza kuipaisha CRDB kama angekuwa amesomea masuala ya nyuklia alafu akapewa CRDB au aliyesomea ‘shipping’akapelekwa hospitali kutibu wagonjwa lazima ataua watu, ndio kilichopo kwa sasa kwenye fani hii ya usafirishaji kwa njia ya meli.” amesema na kuongeza

“Shipping ni mishipa ya damu ya uchumi wa taifa, na watalaam wa meli wako pembeni, sio kwamba wanapenda, hapana, asilimia 90 ya mizigo inachukuliwa na meli.

“Ni wakati sasa wa serikali kuitangaza taaluma kwenye soko la ajira kama zilivyo taaluma kwa kuwa ukiingia kwenye ajira Portal utakuta transport and logistics, shipping imewekwa kwenye kapu moja na transport inapaswa kujitegemea,” amesema

Kuhusu kitabu hicho amesema ameandika kama kutoa huduma,na kwamba  kitasaidia wanafunzi, watunga sera, wateja na wadau wengine wa shiping ikiwemo TRA.

“Wapo wanaosema shiping ni wezi, hapana Mungu alibariki watu wanaofanya kazi za bahari, ndio maana watu wake wanakuwa na hela tena dola, Zaburi 123 hadi 125. Zaburi inasema watu wanaoshughulika na maji lazima wawe na fedha za kutosha

Naye, Mbunge wa Vunjo, Dk.Charles Kimei ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo amesema kitabu hicho kimeandikwa kwa lugha rahisi na kwamba sekta ya usafirishaji kwa njia ya meli ni muhimu.

“Julius ni Mtanzania wa kwanza kuandika kitabu cha ‘shipping’ ni mtu wa maana sana, leo hii amekuja na kitu cha kuweka mezani. Yeyote anayetaka kuingia katika sekta hiyo ni vema akawa na kitabu hicho kwani kinaelezea hatua kwa hatua jinsi ambavyo mizigo inasafirishwa kwa njia ya meli na kwamba katika bahari kuna fedha.

Hata hivyo kitabu hicho kinaelezea mchakato gani unakuwepo katika kupakia mzigo kutoka eneo moja kwenda nyingine, sheria zipi zinazotumika kuhakikisha mzigo unasafiri kwa haraka.

Ukweli hicho kitabu hicho katika kila kurasa kuna maswali ya kujiuliza,hivyo ni kizuri sana.Nafikiri kitabu hicho ukiwa nacho katika meza hakuna sababu ya kuwa na kitabu kingine.

Amesema wengine huko nyuma walikwenda katika shipping kwa kujifunza kwa kujaribu, kitabu hicho kinafafanua jinsi ya kuagiza mzigo,kutoa mzigo na wakati mwingine ukiwa nacho huna sababu ya kwenda kwingine.

Kitabu kinaingia katika soko, mtu unaposoma na kuelewa hiyo field moja, wataona fursa zipo, kinachowezesha uchumi kukua ni uchumi wa blue.

Katika bandari kuna rangi nne, green, blue, yellow,black ambayo ni sisi watu wafanya kazi wazuri, Kilimo hatukufanikiwa.

Lakini viongozi wetu wamekuja na uchumi wa buluu maana katika kilimo mvua hakuna, sasa tunahitaji uchumi wa buluu ambao utapeleka katika maendeleo, ndio wakati wa kutumia vizuri bandari zetu.

Wanasema shilingi moja unayoweka katika uchumi inakupa asilimia tano ya uchumi unaopatikana katika kilimo. Sio kwamba kilimo sio kizuri hapana bali umefika wakati kuhamasisha vijana kujikita katika uchumi wa buluu.

Anasema katika bahari huwezi kukosa samaki mmoja hata kama unamtukana Mungu.

“Tutumie bahari kujenga uchumi wa bluu, tuwe na meli ambazo zitakuwa na migahawa, sasa hivi tunajivunia kabisa kwamba viongozi wameona haja ya kwenda katika uchumi wa buluu.

Bandari ya Dar es Salaam  imeboreshwa na meli zimeanza kuja kubwa ambazo zinakuwa na mzigo mkubwa, badala ya kuwa na vimeli vidogo.

“Bandari ya Bagamoyo, mazungumzo yameanza tena,tutaanza kuona bandari ya Bagamoyo itakuja na mambo mengi, naamini kitu ambacho kinatoa matumaini uchumi wetu utaendelea kukua, bandari ya Tanga nayo imeanza kuchimbwa, Mtwara nako uboreshaji unaendelea,kuna dhamira ya kuwa na uchumi endelevu wa kimazingira .

Amesikia malalamiko yaliyopo ni miundombinu ya reli ya SGR  lazima ikamilike ili kurahisisha usafirishaji sambamba na kuboresha reli ya Tazara.

Aidha Kemei amesema Shirika la Uwakala wa Meli (TASAC), asiwe mshindani katika biashara.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/af63a299b4c1b1c85492e900a1d93497.jpg

SERIKALI imepanga kujenga ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi