loader
Dstv Habarileo  Mobile
Makalla: Wanaume vitonga ‘Mario’ wananyanyaswa

Makalla: Wanaume vitonga ‘Mario’ wananyanyaswa

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amesema wanaume wapenda vitonga maarufu ‘Mario’ wamekuwa wakifika ofisini kwake na kulalamika kuonewa na wanawake zao.

Makalla ameyasema hayo leo katika uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Ee mwananchi, komesha ukatili wa kijinsia sasa’.

“Kwenye kero nilizozikuta wapo wanaume wanaonyanyaswa. Kuna wanawake wana fedha wanahitaji tu wanaume wa kuwaoa, hivyo anaweza kumpa kitu mwanaume na kumnyang’anya punde wakiachana,” amesema Makala.

Amesema sasa hivi wanaume wamekuwa na malalamiko mengi  dhidi ya wanawake wenye fedha.

Amesema pamoja na kupokea kero za wanawake wanaokutana na unyanyasaji wa kijinsia wapo wanaume pia wanaohitaji msaada kutokana na changamoto za aina hiyo.

“Nilikuwa na ziara ya kusikiliza kero za wananchi, asilimia  30 ya kero 927 nilizopokea zinatokana na changamoto za ukatili na unyanyasaji wa kijinsia.

Mkuu huyo wa Mkoa ameongeza, “Nimeyaona hayo wale wanaume marioo waliozoea kitonga  wanakuja ofisini kulalamika kuwa walipewa mali na wanawake lakini wakanyang’anywa.

“Sasa swali linakuja hii sio ukatili? Naona kuna mjadala mpana katika hili suala la unyanyasaji wa kijinsia ndio mana mjadala mzuri wenye lengo la kuboresha sheria za ndoa,”.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/8881ae22701dc839071bab02be24a242.jpg

SERIKALI imepanga kujenga ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi