loader
Dstv Habarileo  Mobile
Mwongozo madawati ya jinsia vyuo vikuu, vya kati wazinduliwa

Mwongozo madawati ya jinsia vyuo vikuu, vya kati wazinduliwa

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa leo amezindua mwongozo wa uanzishwaji wa madawati ya jinsia kwenye vyuo vikuu na vya kati.

Mwongozo huo unalenga kukomesha vitendo vya rushwa ya ngono vinavyoelezwa kushamiri kwenye taasisi za elimu ya juu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya siku 16, Majaliwa amesema nguvu kubwa inatakiwa kuongezwa katika kukabiliana na tatizo hilo ambalo linaathiri vijana wengi wa kike.

Majaliwa amesema vita dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia inapaswa kushirikisha watu wote wanaochukia vitendo hivyo.

Amesema hatua  ya kuanzishwa kwa mwongozo inaweza kuwa mwarobaini wa kumaliza tatizo hili la unyanyasaji kwa mabinti waliopo vyuoni.

Amesema taasisi za elimu ya juu  ni maeneo ambayo mara kadhaa serikali  imekuwa ikipata  taarifa za uwepo wa vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia.

“Tunahitaji watanzania kuthamini maisha ya kila mmoja wetu, tunataka kila mtanzania awe huru, anayesoma asome kwa uhuru.

“Naendelea kusisitiza uanzishwaji wa madawati ya jinsia kwenye vyuo vyote. Hii ni ajenda na ilani ya CCM imesisitiza haki na usawa na kuwalinda watanzania dhidi ya ukatili wa kijinsia.

Aidha ametumia fursa hiyo kuwataka wadau wa masuala ya jinsia kutumia siku 16 kujadili mapungufu yaliyopo kwenye sheria ili zifanyiwe maboresho.

“Maboresha haya yakiletwa yatafanyiwa kazi kwa haraka yakifika bungeni, tunataka watanzania wote waishi kwa matumaini makubwa,” amesema Majaliwa.

Nae Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mwanaidi Ali Hamis, alisema tizo la ukatili wa kijinsi kwa wanawake linaendelea kuwepo kwa sababu ya baadhi yao kuficha madhira wanayokutana nayo.

Amesema endapo kila mwanamke anayepata changamoto ya ukatili wa kijinsia akiondoa ukimya tatizo hilo  litakwisha.

“Mkijificha au kuficha vitendo vya ukatili wa kijinsia mnamuangusha rais wetu kwa kuwa yeye anataka wanawake tupate maendeleo.

“Wizara itaendelea kuhakikisha kamati zote za ulinzi wa wanawake na watoto zinaundwa ili kutoa nafasi kwa watu kuzitumia.

Pia tutaendelea  kusimamia na kutengeneza sera, sheria na miongozo ambayo inalenga kukomesha vitendo hivi,” amesema Mwananidi

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/2705cc251c680a979ed52f36f6e3b27f.jpg

SERIKALI imepanga kujenga ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi